(Wimbo ulio Bora 1:5-6)
UTANGULIZI
Ukweli ni kwamba kila mwanamke ana uzuri wake lakini shetani amekuwa akifanya vita za aina mbalimbali dhidi ya wanawake ikiwemo vita dhidi ya uzuri wa mwanamke.
Ukisoma kitabu cha (Wimbo ulio Bora 1:5-6) huyu mwanamke anasema "yeye ni mweusi mweusi ila anao uzuri"
Habari hiyo inatujulisha kuwa WATU WALIKUWA WANAONA WEUSI WAKE ILA WALIKUWA HAWAONI UZURI WAKE ndio maana anajisemea mwenyewe kwamba yeye ni mweusi ila anao uzuri.
Huyu mwanamke anaeleza kilichosababisha uzuri wake kutoonekana ni kazi ngumu aliyopewa kuifanya (Wimbo ulio Bora 1:6)
VITA DHIDI YA UZURI WA MWANAMKE
Shetani huhakikisha anaficha uzuri wa mwanamke usionekane pia anaharibu uzuri wa mwanamke kwa njia mbalimbali kwa kuwa anajua uzuri wa mwanamke una mchango mkubwa sana kwenye maisha yake ikiwemo KUMFANYA MWANAMKE AWE NA MVUTO NA APATE MUME WA KUMUOA.
Njia mojawapo ambayo shetani huitumia kuharibu uzuri wa mwanamke ni kuhakikisha mwanamke anapata kazi ngumu au anafanya kazi ngumu (Wimbo ulio Bora 1:6), kazi ngumu huharibu ngozi ya mwanamke, umbo lake nakadhalika.
Pia shetani huutumia uzuri wa mwanamke kama fursa yake ya kumfanya mwanamke awe na kiburi, dharau nakadhalika ndio maana si ajabu kusikia watu wakisema fulani ni mwanamke mzuri ila ana kiburi na dharau kwa hiyo wanaume hawawezi kumuoa mwanamke mwenye kiburi na dharau. Wanawake wengi wakishajigundua ni waziri huanza kusumbuliwa na kiburi na dharau, wengine hujikuta wanatumiwa na shetani kufanya mambo mabaya kutokana na nguvu ya uzuri wao. Uzuri ulimfanya Malkia Vashti akawa na kiburi hata alipoitwa na Mfalme Ahasuero ambaye alikuwa mumewe ili watu waone uzuri wake alikataa kuja kwa sababu ya kiburi (Esta 1:10-12)
Uzuri wa mwanamke ni fursa yake ambayo Mungu amempa imsaidie katika mambo mbalimbali ikiwemo kupata mtu wa kumuoa.
Kilichomfanya Adamu akamfurahia Eva baada ya kuumbwa ni uzuri wa Eva mpaka Adamu akasema "huyu ni nyama katika nyama zangu mfupa katika mifupa yangu" hiyo ni kauli ya mtu aliyevutiwa na mwanamke.
Mama yetu Sara alipoingia nchini Misri wanaume waliuona uzuri wake mpaka wakamsifia mbele ya Mfalme Farao hatimaye Farao akamchukua Sara ili awe mkewe, Mungu akazuia Sara asiolewe na Mfalme Farao, kilichosababisha hayo yote ni uzuri wa Sara (Mwanzo 12:10-20).
KWA NINI SHETANI ANAPAMBANA NA UZURI WA MWANAMKE
1. Uzuri wa mwanamke ni nguvu mojawapo ya mwanamke.
2. Uzuri wa mwanamke ni fursa ya mwanamke ya kumsaidia mambo mbalimbali ikiwemo kusababisha apate mume wa kumuoa.
BAADHI YA MBINU ZA KUSHINDA VITA DHIDI YA UZURI
1. Epuka kazi ngumu.
2. Vaa vizuri upendeze.
3. Omba Mungu aufunue uzuri wako na akushindie dhidi ya vita hivi.
0 Maoni