KUJIKUBALI


 Tatizo mojawapo linalowatesa watu wengi sana duniani ni tatizo la kutojikubali, tatizo hili ukilitazama kibinadamu ni tatizo la kisaikolojia lakini ukilitazama kutokea kwenye neno la Mungu ni tatizo la kiroho.

Kutojikubali kumesababisha watu wengi sana kufanya mambo ya ovyo kabisa kama vile;

1. Kubadili jinsia.

2. Kubadili rangi ya ngozi.

3. Kuvaa mavazi yasiyo rafiki kutegemeana na aina ya mwili wa mtu.

4. Wanawake kutaka kuwa kama wanaume na wanaume kutaka kuwa kama wanawake.

Nakadhalika.

Kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa Mungu sio mpumbavu aliyeamua uwe mwanamke au mwanamume, Mungu sio mpumbavu aliyeamua uwe na makalio madogo au makubwa, Mungu sio mpumbavu aliyeamua uzaliwe Afrika au nchi fulani, MUNGU SIO MPUMBAVU.

Isipofika hatua ukajikubali basi utajipata kwenye mitego ya shetani inayoleta uharibifu na mauti, JIKUBALI SASA.

JIFUNZE KUTOKA KWENYE MIFANO HII

1. Daudi (Zaburi 139:14)

Daudi alisema "Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana"

2. Wimbo ulio bora 1:5

 "Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani" 

Nakusisitiza jikubali, mshukuru Mungu kwa jinsi alivyokuumba.

Chapisha Maoni

0 Maoni