Ni makosa
kufiiri muda unaenda. Muda hauendi. Muda upo hapa mpaka mwisho wa dunia. Ni
wewe ndio unaenda. Haupotezi muda, muda hauna mwisho. Unajipoteza mwenyewe,
wewe una mwisho. Ni wewe unayezeeka, muda hauzeeki. hivyo tumia mda wako
vizuri.
Namna mbaya
sana ya kupoteza muda wako ni kujifananisha na wengine. Ng'ombe anakula majani
na ananenepa, lakini Mbwa akila majani atakufa. Kamwe usijilinganishe na
wengine. Kimbia mbio yako. Kinachomfaa mwingine kinaweza kisimfae mwingine.
Tazama zaidi
zawadi na kipawa alichokupa Mungu, na usiwe na wivu juu ya baraka walizopewa
wengine.
Kama ua rozi
linanukia vizuri zaidi kuliko nyanya, haimaanishi kuwa rozi litatengeneza supu
nzuri zaidi. Usijaribu kujilinganisha na wengine.
Pia una uwezo
wako, utafute na ujijengee uwezo zaidi.
Wanyama wote
duniani walikuwa kwenye safina ya Nuhu, na konokono ni mmoja wapo, Kama Mungu
aliweza kumsubiri mpaka konokono aingie kwenye safina ndipo afunge mlango,
mlango wako wa neema kamwe hauwezi ukafunga kwako mpaka ufike mwisho, siku zote
mtegemee yeye.
Kamwe
usijidharau, endelea kusonga mbele. Kumbuka
kuwa rangi zilizovunjika, bado zinachora.
0 Maoni