Faraja Gasto
Utangulizi
(Ayubu 22:21)
“Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia”
Kati ya vitu ambavyo kila mtu anatakiwa kuvipa
kipaumbele, jambo mojawapo ni KUMJUA MUNGU, Kuna faida nyingi sana za kumjua
Mungu wewe binafsi.
Unapomjua Mungu unapata AMANI, hiyo amani unayopata ina
kazi kubwa sana kwenye maisha yako.
Zipo faida nyingi sana za kumjua Mungu, ila napenda
kujikita kuzungumzia faida kuu mbili.
FAIDA ZA KUMJUA MUNGU
1.Itakusaidia
kufanya maamuzi bila KUTAFUTA USHAURI KWA MTU AU WATU
Suala la kufanya
maamuzi lipo katika maisha yetu ya kila siku, kila iitwapo leo kuna maamuzi
unatakiwa uyafanye kwa mfano ule nini, umuoe nani, uolewe na nani, ushirikiane
na nani, utoe au usitoe n.k kwa hiyo hayo ni baadhi ya mambo ambayo unatakiwa
kuyafanyia maamuzi.
Katika kufanya
maamuzi kuna wakati akili za mtu huwa zinafikia ukomo hapo ndipo huwa linakuja
suala la kutafuta washuri wa nje (external advisor).
Biblia inasema “Mjue
sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia” kazi mojawapo ya hiyo amani ni
kukusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu mambo mbalimbali, hiyo amani ITAAMUA
kwa niaba yako na inapoamua kwa niaba yako haina haja ya kutafuta washauri wa
nje kwa kuwa ndani yako yako utakuwa unajisikia hiyo amani ikitawala unapofanya
maamuzi, hautabiki njia panda katika kufanya maamuzi.
Haujawahi kusikia binti anamuomba ushauri binti mwenzake
kuwa “Kuna vijana wameniambia wanataka kunioa sasa niko njia panda sijui
nimkubalie nani” hali ya kubaki njia panda inatokana na KUTOMJUA MUNGU, ukimjua
Mungu hautabaki njia panda, ukimjua Mungu unakuwa na amani katika maamuzi yako.
Angalizo:
Kutafuta au kuomba ushauri kwa watu wengine sio vibaya ila lazima uwe na
tahadhari unaomba ushauri kwa nani, kwa wakati gani, ushauri juu ya nini.
USISAHAU HILI: Ukiona
inafika hatua UNABAKI NJIA PANDA HAUJUI UFANYE NINI, fahamu kuwa kuna ufahamu
wa KiMUNGU umekosa katika fahamu zako, ndio maana nakuambia tafuta kumjua
Mungu.
2.Itakutengenezea
UJASIRI katika kuzungumza habari za Mungu na katika KUAMINI
(Danieli
3:1-25)
Kuna uhusiano kati ya
UFAHAMU na UJASIRI, kama haufahamu kitu fulani unakosa ujasiri wa kuzungumza
hicho kitu, kwa hiyo kama unakosa ujasiri wa kuzungumza habari za Mungu maana
yake ni kwamba umekosa ufahamu kuhusu Mungu (haumjui Mungu sawasawa)
Kuna uhusiano kati ya
UFAHAMU na IMANI, kama haufahamu jambo fulani unakosa imani juu ya jambo hilo,
kwa mfano kama kama haufahamu habari za Yesu basi hauwezi kuamini habari za
Yesu. Kwa hiyo kuna uhusiano kati ya UFAHAMU na IMANI.
Wapo watu wengi sana
hawana ujasiri katika imani zao kwa sababu ya KUTOKUMJUA MUNGU, ujasiri upo wa
aina nyingi, kuna ujasiri wa kuongea, kuna ujasiri wa kufanya jambo, ujasiri wa
kuamini…………
Ukimjua Mungu unakuwa
na ujasiri kwenye imani yako kwa hiyo huwezi kuwa na mashaka maana una ujasiri
kuwa kile unachoamini ndicho kitatokea.
Ukisoma hilo andiko
(Danieli 3:1-25) utaona hao vijana watatu walikuwa WANAMJUA MUNGU, kule kumjua
MUNGU kuliwasaidia kuwa na UJASIRI katika kuzngumza kuhusu MUNGU wao na pia
UJASIRI katika KUMUAMINI MUNGU WAO.
IKO HIVI: PALE
UFAHAMU WAKO UNAPOISHIA NDIPO UJASIRI WAKO UNAPOISHIA NA NDIPO IMANI YAKO
INAPOISHIA NA NDIPO UHURU WAKO UNAPOISHIA.
NINAWEZAJE
KUMJUA MUNGU?
Hilo
swali ni la msingi sana name nahitaji kulijibu kwa namna hii
1. 1. Mpokee
Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako (Hii ni kwa ajili ya wale ambao
hawajampokea Yesu).
Unaweza
ukajiuliza kunauhusiano gani kati ya Yesu na Mungu
JIBU
NI HILI: YESU NDIYE SURA YA MUNGU
Biblia
inasema “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini,
isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo
aliye sura yake Mungu”. (2 Wakorintho 4:4)
2. 2. Soma
habari zake kwenye kwenye Biblia na kwenye vitabu vya watumishi wa Mungu
(Wakolosai 3:16-17)
Kuna msemo unasema
“Kusoma ni kusafiri” kwa hiyo unaposoma habari za Mungu unakwenda moja kwa moja
kwa Mungu unaanza kumuona katika fahamu zako, unaanza kuhisi uwepo wake n.k
3. 3. Omba
Mungu akupe “roho ya hekima” na “roho ya ufunuo” ili uweze kumjua kwa marefu,
mapana n.k na pia omba Mungu ayatie nuru
macho yako
(Waefeso 1:17-18)
2 Maoni
Amina nimependa
JibuFutaKweli kumjua Mungu Kuna faida kubwa Sana .Mungu Katuumba na ndiye atupaye Maisha.Ukweli kuhusu Maisha ni Kumjua Mungu,kulishika Neno lake na Kutenda mapenzi Yake.
JibuFuta