WATU WA KUKUPENDA


 Mungu mwenyewe anataka kupendwa? WEWE NI NANI  USIYETAKA KUPENDWA?🤷 au haujawahi kusoma haya maandiko (Kumbukumbu la torati 10:12)(Mathayo 22:37)(Yohana 21:15-17).

Wakati mwingine muombe Mungu akuinulie watu wa kukupenda.

Mungu alimpa Daudi mtu wa kumpenda aliyeitwa Jonathani mtoto wa Mfalme Sauli (1 Samweli 18:1-4)

Kutokana na upendo aliokuwa nao Jonathani  kwa Daudi, Jonathani alivujisha taarifa za mipango iliyopangwa na Mfalme, mipango ya kumuangamiza Daudi (1 Samweli 19:1-7), Daudi alinufaika sana na upendo huo.

Jonathani alipokufa, Daudi wakati huo alikuwa Mfalme aliomboleza sana, soma maelezo ya maneno ya maombolezo ya Mfalme Daudi kuhusu Jonathani.

2 Samweli 1:26. Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; UPENDO WAKO KWANGU ULIKUWA WA AJABU, KUPITA UPENDO WA WANAWAKE. 

✓Ni kweli hutapendwa na kila mtu ila UKIKOSA WATU WA KUKUPENDA UTAKOMA.

✓ Wakati mwingine muombe Mungu akuinulie watu wa kukupenda.

Chapisha Maoni

0 Maoni