MWANA WA PEKEE


(Yohana 3:16)


UTANGULIZI


Mungu anao wana wengi lakini katika hao wengi yupo mmoja wa pekee anaitwa Yesu Kristo.


Yapo mambo mbalimbali yanayomfanya Yesu kuwa wa pekee, nataka tujue mambo kadhaa kwa nini Yesu awe mwana wa pekee.


UPEKEE WA YESU

✓ Vitu vyote viliumbwa kupitia yeye, pasipo yeye hakuna chochote kilichofanyika (Yohana 1:1-3)


✓Maombi yanajibiwa tukiomba kwa jina lake tu (Yohana 16:23-24).


✓Jina la Yesu ndilo linamfanya Mungu apate watoto, Kila anayeamini jina la Yesu anafanyika kuwa mtoto wa Mungu (Yohana 1:12)


✓Damu yake ndio inayoondoa dhambi (Mathayo 26:28)


✓Alizaliwa na bikira kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Luka 1:26-35)


✓Yesu ni Mungu, Mungu mwana (1 Yohana 5:8)(Wafilipi 1:5-6)


✓Yesu Kristo ndiye sura ya Mungu Baba (2 Wakorintho 4:4)


✓Jina la Yesu ni tishio kwa nguvu zote za giza ikiwemo majini au pepo, magonjwa, uchawi nakadhalika (Marko 16:17-18)


HITIMISHO

Baada ya kuona kwa ufupi upekee wa Yesu, Kila mmoja hapaswi kumchukulia Yesu kuwa wa kawaida kama wengine wanavyomchukulia, Yesu ni zaidi ya malaika (Waebrania 1:4).


Yesu ni Bwana wa mabwana ni Mfalme wa Wafalme, Yesu ni mwokozi wa ulimwengu.

Chapisha Maoni

0 Maoni