Utangulizi
Mungu amekuwa akikutana na watu mbalimbali kwa namna mbalimbali, Mungu alipokutana na watu kuna mambo mbalimbali yalitokea ambayo nataka tuyafahamu ili tujifunze umuhimu wa Mungu kukutana na mtu.
Nini hutokea watu wanapokutana na Mungu?
1. Watu hubadilika
Watu hubadilika kitabia, muonekano, usemi, mitazamo nakadhalika.
(Matendo ya mitume 9:1-22)
Sauli alikuwa tishio kwa kanisa, kila mahali Sauli alipofika kulikuwa na msiba Kwa kanisa LAKINI ALIPOKUTANA NA MUNGU, Sauli alibadilika kabisa kiroho na kisaikolojia, Sauli aliyekuwa muuaji akaanza kuwa mhubiri wa Injili.
Swali: Kuna mtu amekuwa tishio kwenye familia, mtaa, taifa, kanisa nakadhalika au Kuna mtu ni mtukutu, mkaidi nakadhalika?
Kama jibu ni ndiyo basi MWAMBIE MUNGU AKUTANE NA MTU HUYO AU WATU HAO, Mungu akikutana naye au akikutana nao lazima wabadilike.
(Yohana 4:7-41)
Yesu alipokutana na mwanamke Msamaria, maisha ya yule mwanamke Msamaria yalibadilika siku ile, yule mwanamke akaanza kuhubiri injili katika mji alikokuwa akiishi.
2. Watu hupokea maagizo au maelekezo kutoka kwa Mungu
(Matendo ya mitume 1:4)
Yesu alipokutana na wanafunzi wake aliwaagiza wasitoke Yerusalemu bali wangojee kujazwa Roho Mtakatifu.
(Kutoka 3:1-14)
Musa alipokutana na Mungu ndipo alipewa maelekezo ya kwenda kuwatoa wana wa Israeli katika utumwa pale Misri.
0 Maoni