MTUMISHI NA MKE WAKE


 Watumishi wa Mungu wengi wamejikuta kwenye vipindi vigumu kiutumishi, kiusalama, kimahusiano na watu na kimaamuzi kutokana na kuwaambia wake zao kila jambo au kuwashirikisha wake zao kila jambo kwa madai kuwa wao ni mwili mmoja. 

Ukweli ni kwamba kuwa mwili mmoja haimaanishi unapaswa kumwambia mkeo kila jambo au kumshirikisha mkeo kila jambo, unapokuwa mtumishi wa Mungu uko vitani na shetani lazima uchukue tahadhari katika taarifa unazomwambia au unazomshirikisha mkeo, si kila jambo unapaswa kumwambia mkeo au kumshirikisha mkeo MAMBO MENGINE YANAKUHUSU WEWE MWENYEWE.

Kwa mfano, fikiria kama Ibrahimu angemwambia mkewe Sara kwamba Mungu amemwambia akamtoe Isaka kama sadaka ya kuteketezwa, ni dhahiri kuwa ndoa yao ingeingia kwenye wakati mgumu kwa kuwa isingekuwa rahisi Sara kukubaliana na mumewe kumtoa Isaka. Ibrahimu aliondoka kwenda kumtoa Isaka kama sadaka huku mkewe hajui kinachoendelea (Mwanzo 22:1-19)

Kwa mfano ukisoma Biblia utagundua kilichosababisha shujaa Samsoni akapatwa na matatizo ni kumwambia mwanamke (Delila) jambo ambalo hakupaswa kumwambia (Waamuzi 26:16-21)

Mtumishi wa Mungu Nabii Mika alisema hivi 

"Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari" Mika 7:5.

MSISITIZO: Sijasema uwe unamficha mkeo mambo ila nafundisha kuwa kama wewe ni mtumishi wa Mungu usimshirikishe mkeo kila jambo (usimwambie mkeo kila jambo).

Chapisha Maoni

0 Maoni