NAMNA YA KUMTUMIA MTU AU WATU AMBAO WANAWEZA KUKUFANYA UFANIKIWE

Faraja Gasto

Utangulizi

WATU wanatajwa kama rasilimali (resource), kwa hiyo ndani ya watu kuna vitu vingi sana ambavyo unaweza ukavipata endapo utajua namna ya kuwatumia.
Ndani ya mtu kuna vitu vingi hivi ni baadhi
(a)Maarifa-Elimu  (b) Ujuzi
(c)Taarifa (d)Kipaji au vipaji

ANGALIZO: Si kila mtu ana kitu cha kukufaa wewe kwa hiyo lazima uwe na tahadhari unapofanya maamuzi ya kuwa karibu na mtu fulani. Lazima kwanza uangalie wewe unataka kufanikiwa katika eneo gani hiyo itakusaidia kufahamu aina ya watu unaotakiwa kuwa nao karibu.

Vitu kadhaa ambavyo utavipata endapo utafahamu namna ya kuwatumia watu
1.Maarifa (Knowledge)
2.Kuunganishwa na watu wengine wa muhimu kwako (connection)
3.Fedha
Fedha ni nini?
Kwa haraka haraka unaweza kusema fedha ni sarafu au noti.
Lakini si hivyo tu, Kwa mujibu wa wana uchumi, FEDHA NI KITU CHOCHOTE CHENYE THAMANI (Anything which has value)
Kwa hiyo meza ni fedha, wewe ni fedha, simu ni fedha n.k

MAMBO YATAKAYOKUFANYA UFAHAMU NAMNA YA KUWATUMIA WATU ILI UFANIKIWE

1.Jiunganishe nao (KUWA NAO KARIBU)
--Omba mawasiliano yao (namba za simu, e-mail n.k)
--Wasiliana nao ili ubadilishane nao mawazo n.k
ANGALIZO : Jihadhari usiwe kero kwao kwa mfano unaweza kukuta wengine ni waume au wake za watu kwa hiyo lazima uwe makini katika kuwasiliana nao.

2. Fahamu WANACHOFANYA na jinsi WANAVYOFANYA
--Fuatilia wanachofanya na wanavofanya, fahamu kuwa unaweza ukamfuatilia mtu UKAJUA ANACHOFANYA ila USIJUE NAMNA ANAVYOFANYA kwa hiyo usiishie tu kujua anachofanya bali JIFUNZE NAMNA ANAVYOFANYA.
Kama unataka kufanikiwa katika biashara fulani, fuatilia wanaofanya hiyo biashara ili ujue wanachofanya na wanavyofanya.

3.Waulize maswali
--Ukipata nafasi ya kuwauliza maswali waulize maswali.
Unapouliza maswali unaifanya mioyo yao ifunguke iachilie vitu kwako (uzoefu wao, changamoto walizopitia n.k)
FAHAMU KUWA: Kuna watu kwa sababu wanazozijua wao huwa wanajiona kuwa wanafahamu kila kitu (UJUAJI-MUCH KNOW)
Ujuaji ni kitu kibaya sana kwenye maisha, siku zote mtu anayejifanya kuwa anafahamu kila kitu huwa hafiki mbali (ni vigumu kufanikiwa)
Kwa hiyo ni vema ujifunze “kujifanya mjinga” jifunze kuuliza maswali hii itakusaidia kugundua vitu vingi sana.

4. Waajiri (Hii ni kwa ajili ya watu wenye mashirika, taasisi na  makampuni)
àKama una uwezo wa kuwajiri waajiri katika kampuni yako, taasisi yako, shirika lako n.k.
àKama unaona mtu fulani ana kitu cha kuifaa taasisi yako, shirika lako au kampuni yako kubali kuingia gharama ya KUMUAJIRI ili autumie ujuzi wake au ufahamu wake kusitawisha taasisi yako, kampuni yako au shirika lako.

5.Wape nafasi ya kufanya kile wanachoweza kufanya ambacho kina manufaa kwako
--Fahamu kuwa kila mtu una kitu anaweza kukifanya ila si kila ambacho watu wanakifanya kina manufaa kwako.
Kuna watu wana vitu ndani yao lakini hawana nafasi ya kuvitoa nje unapowapa nafasi maana yake unauhusu vilivyomo ndani yao vitoke.






Chapisha Maoni

0 Maoni