"nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila NENO LILILO KUBWA WATAKULETEA WEWE, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe"
Kwenye kila taifa Mungu huweka au huinua mtu au watu wa kubeba mambo makubwa makubwa mtu huyo anaweza kuwa Mfalme, Rais wa nchi, mwanasiasa fulani, mfanyabiashara au kiongozi wa kiroho nakadhalika.
Musa ni miongoni mwa watu waliopewa neema ya kubeba mambo makubwa makubwa Kwa maslahi ya taifa, Mungu alipitisha neno la hekima Kwa baba mkwe wa Musa ili kumjulisha Musa HAPASWI KUSHUGHULIKA NA MAMBO MADOGO MADOGO BALI ANAPASWA KUSHUGHULIKA NA MAMBO MAKUBWA MAKUBWA.
TANZANIA
Kuna watu Mungu amewaweka hapa Tanzania kushughulika na mambo makubwa, kuna wengine ni wanasiasa katika chama tawala wengine ni wanasiasa katika vyama vya upinzani, wengine ni wabobezi wa taaluma fulani, wengine ni viongozi wa kiroho kama vile Bishop Dr Josephat Gwajima nakadhalika.
Hivyo basi tuendelee kuwabeba kwa maombi ili mikono yao itiwe nguvu pia waokolewe na watu wabaya wasiolitakia mema taifa letu.
ANGALIZO: Kama Mungu hajakuitia mambo makubwa USING'ANG'ANIE KUSHUGHULIKA NA MAMBO MAKUBWA, kama Mungu amekuitia mambo makubwa USIHANGAIKE NA MAMBO MADOGO, kama Mungu hajakupa nafasi inayokuwezesha kushughulika na mambo makubwa USIHANGAIKE NA MAMBO MAKUBWA UTAUMIA.
0 Maoni