(Wagalatia 6:9-10)
Yako mambo mbalimbali yanayosababisha watu waache kutenda mema, mambo baadhi ni kama vile;-
1.Kulipwa mabaya badala ya mema.
2.Kutokea mambo ambayo haukuyatarajia, kwa mfano mtu ametenda mema akitarajia aliyetendewa mema atamshukuru lakini aliyetendewa akaacha kushukuru.
3.Majeraha ya moyo, kwa mfano mtu alimtendea mema mtu fulani lakini yule aliyetendewa mema akalipa mabaya, moyo wa aliyetenda mema hujeruhika.
NB: Pamoja na yote hayo Mungu anatutaka tusichoke kutenda mema.
KWA NINI UTENDE MEMA
1.Uliumbwa utende matendo mema tu (Waefeso 2:10)
-Kutenda mema ni asili pia ni tabia ya Mungu ambayo mtu aliumbwa nayo ndani yake.
2.Matendo ni mbegu utakayovuna, ukitenda mabaya utavuna mabaya, ukitenda mema utavuna mema (Wagalatia 6:9-10).
3.Atendaye mema ni wa Mungu (3 Yohana 1:11)
HITIMISHO
Ukitendewa mabaya usilipe mabaya, Mungu anataka usichoke kutenda mema ila ameweka kipaumbele ambacho ni "Waliookoka" yaani unapaswa kuwatendea mema waliookoka kwa kiwango kikubwa zaidi ya ambao hawajaokoka (Wagalatia 6:10).
0 Maoni