NGOME IMARA


 UTANGULIZI

Kumekuwepo na vita hapa duniani, vita kati ya nchi na nchi, kati ya kundi na kundi nakadhalika.

Tumekuwa tunashuhudia watu wakikimbia kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine ili kukwepa vita (wakimbizi).

Vivyo hivyo katika vita vya kiroho kuna mahali pa kukimbilia ili uwe salama, mahali pa kukimbilia ni KWENYE NGOME.

NGOME NI IPI?

NGOME yenyewe ni jina la Bwana 

(Mithali 18:10)Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama. 

Unapolikimbilia jina la Bwana unakuwa salama dhidi ya mashambulizi ya kiroho.

Je! unahitaji kuwa salama dhidi ya mashambulizi ya kiroho kutoka kwa shetani na ufalme wake? 

Kimbilia kwenye jina la Bwana, kama haujamwamini Yesu hakikisha unamwamini Yesu ili kupata haki ya kukimbilia kwenye ngome ambayo ni jina la Bwana.

Mtu mwenye sifa za kukimbilia kwenye ngome ni mwenye haki "mwenye haki huikimbilia akawa salama" 

Utahesabiwa kuwa mwenye haki kwa kumwamini Yesu 

(Warumi 3:24)

wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.


Chapisha Maoni

0 Maoni