KUHUBIRI KILA SIKU


 (1 Mambo ya nyakati 16:23-24)(Zaburi 96:2)

Mapenzi ya Mungu ni kuona watu wanaokolewa kila siku, hivyo basi ili watu waokolewe kila siku lazima tujifunze na tuamue kuhubiri kila siku  kwa kuwa mahubiri yana nafasi kubwa ya kuwafanya watu kuamini (Warumi 10:14)

Kanisa la Yerusalemu liliongezeka kila siku kwa kuwa watu waliokoka (Matendo ya mitume 2:47)

Kama watu waliokoka kila siku maana yake ni kwamba injili ilihubiriwa kila siku (Matendo ya mitume 5:42)

Mtume Paulo alihubiri kila siku (Matendo ya mitume 17:17)(Matendo ya mitume 19:9)

KWA NINI TUHUBIRI KILA SIKU?

1. Kuna uwezekano watu kuokoka kila siku (Matendo ya mitume 2:47)

- Kama kanisa liliongezeka kila kutokana na watu wanaookoka basi kuna uwezekano watu kuokoka kila siku.

2. Kila siku tunakutana na watu, kama tunakutana na watu kila siku basi kuna uwezekano wa kuhubiri kila siku (Matendo ya mitume 17:17).

3. Kila siku watu wanakufa, wengine wanakufa bila kumwamini Yesu kwa hiyo wako kwenye idadi ya watu wanaotarajia kutupwa jehanamu (Waebrania 9:27)

4. Kila siku Yesu ni mwokozi, anaweza kuokoa watu kila siku iwe usiku au mchana (Matendo ya mitume 2:42)

- Kuna watu waliokoka usiku (Matendo ya mitume 16:32-34) Kuna watu waliokoka mchana (Matendo ya mitume 2:15, 40-41).

5. Injili ni habari njema, watu wanahitaji habari njema.

TUNAWEZAJE KUHUBIRI KILA SIKU?

1. Kuwahubiri watu tunaokutana nao sokoni, njiani, kazini nakadhalika (Matendo ya mitume 17:17).

2. Kuhojiana na watu kila siku kuhusu mambo ya ufalme wa Mungu (Matendo ya mitume 19:9)(Matendo ya mutume 17:17).

3. Kuwakaribisha kanisani kila siku na kuwaambia uzuri wa Yesu.

4. Kutangaza matendo makuu ya Mungu ( Zaburi 96:2-3).

NINI TUHUBIRI KILA SIKU?

1. Tuhubiri ufalme wa Mungu umekaribia (Mathayo 10:7).

2. Tuhubiri matendo makuu ya Mungu (Zaburi 96:2-3).

3. Tuhubiri kile ambacho Roho atakuongoza kuhubiri.

4. Tuhubiri injili (Marko 16:15)

Chapisha Maoni

0 Maoni