UTANGULIZI
Neno "ugumu wa maisha" si neno geni masikioni mwa watu, watu wengine wamekuwa wakisema "maisha ni magumu" au "ninapitia wakati mgumu wa kimaisha"
Ziko sababu mbalimbali ambazo husababisha hali ya maisha kuonekana ngumu ila sababu mojawapo inayoelezwa kwenye Biblia ni UGUMU WA MOYO WA MTU AU WATU WENGINE.
Kuna uhusiano mkubwa wa ugumu wa moyo na ugumu wa maisha.
UHUSIANO WA UGUMU WA MOYO NA UGUMU WA MAISHA
(Kutoka 4:21)(Kutoka 5:1-23)
Moyo wa Mfalme Farao ulipofanywa mgumu wana wa Israeli walijikuta wanaishi maisha magumu sana.
IKO HIVI: Ugumu wa moyo unaweza kumuathiri mtu binafsi na kuwaathiri wengine ndio maana jambo mojawapo ambalo Mungu anazuia, anazuia watu wasiwe na mioyo migumu (Waebrania 3:7-8)
HITIMISHO
Ugumu wa moyo unaweza kuathiri maisha yako na watu wengine hivyo basi ukisikia sauti ya Mungu usiufanye moyo wako kuwa mgumu (Waebrania 3:7-8).
Je! una maisha magumu? kama jibu ni ndio basi shughulikia moyo wako pia muombe Mungu aondoe ugumu wa mioyo ya watu unaokusababishia maisha magumu.
0 Maoni