Kila mtu ameshawahi kupoteza vitu vingi.
Wapo waliopoteza wapendwa wao kutokana na kifo nakadhalika.
Wapo waliopoteza matumaini.
Wapo waliopoteza muelekeo wa maisha, hawajui kesho yao itakuaje.
Wapo waliopoteza fedha, mali n.k
KUPOTEZA kunawaletea watu huzuni, majuto, uchungu, kunaondoa amani nakadhalika.
MUNGU NAYE HUWA ANAPOTEZA NA ANAUMIA SANA ANAPOPOTEZA KITU CHAKE
(Luka 15:1-32)
Katika sura hiyo ya kumi na tano Yesu alitoa mifano kuhusu namna wanadamu wanavyohangaika au kuumia mioyoni wanapopoteza vitu mbalimbali.
Kupitia mifano hiyo alitaka kufikisha ujumbe wake kwa watu ili wajue namna Mungu anavyoumia anapopoteza mtu wake.
Kila mtu ambaye yuko nje ya Yesu Kristo Biblia inamuita ni mpotevu (amepotea njia ya kwenda kwao) (Yohana 3:16)
Inamuumiza Mungu sana kuona watu wamepotea ndio maana anataka watu wake warejee kwake maana yeye ndiye Baba yao.
Rejea kwenu kupitia kumwamini Yesu Kristo ambaye ni njia, kweli na uzima (Yohana 14:6)(Yohana 3:16)
0 Maoni