Ni muhimu sana ujifunze kutamka au kukiri tofauti na hali inavyokulazimisha kukiri au kutamka, Mungu anasema "aliye dhaifu aseme mimi ni hodari" Yoeli 3:10
Watu wengi hawaamini kama nguvu ya kukiri au kutamka inatenda kazi kabisa, na Mungu anafuatilia mambo ambayo watu hutamka au kukiri
(Hesabu 14:26-28)
Aliwaambia wana wa Isareli kuwa "kama walivyonena masikioni mwake ndivyo itakavyokuwa yaani waliyoyatamka yatawapata"
Mungu huyaumba matunda ya midomo (Isaya 57:19)
Hivyo basi jizoeze kukiri au kutamka mambo mazuri hata kama hali halisi haifanani na unavyokiri.
0 Maoni