KUEPUKA MTEGO WA KUJIHESABIA HAKI


 Mambo baadhi ya kukusaidia kuepuka mtego wa kujihesabia haki ni haya yafuatayo;-

1. Fahamu kuwa kama unaweza kukosewa na wengine basi hata wewe unaweza kuwakosea wengine.

2. Jizoeze kujitazama kama mkosaji, usijitazame kama mwenye haki, ukijitazama kama mwenye haki utakapokosea hautakubali kuwa umekosea, utakapokosolewa utaona umevunjiwa heshima.

Ukijitazama kama mkosaji itakuwa rahisi sana kwako kusema "nisamehe au nisameheni au kuwa tayari kukosolewa" pindi itakapoonekana umekosea kwa kuwa ndani yako utakuwa na mtazamo huu "hata mimi nakosea"

Chapisha Maoni

0 Maoni