(1 Yohana 2:14)
Msisitizo: inawezekana kumshinda shetani ukiwa kijana (1Yohana 2:14)
UTANGULIZI
Vijana ni kundi muhimu sana, lina manufaa kwa jamii, taifa, ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani.
SHETANI NI NANI?
●Ni yule malaika aliyewashawishi wenzie kumuasi Mungu, joka wa zamani (Ufunuo 12:7-9)
●Ni chochote kinachotokana na shetani au kinachohusiana na shetani.
Yafuatayo ni mambo yanayotokana na kuhusiana na shetani;-
(a). Mawazo ya kishetani (Mathayo 16:23)
(b). Tabia za kishetani (Waefeso 2:3)(Yakobo 3:15(Marko 5:5)
(c). Mawakala au mawakili wa shetani au wajumbe wa shetani.
-Yezebeli alikuwa mjumbe wa shetani ili kumuharibu Mfalme Ahabu na taifa kwa ujumla (1 Wafalme 21:25)
-Delila alikuwa wakala wa shetani ili kumuangamiza Samsoni (Waamuzi 16:18-20)
-Mke wa Potifa alitumiwa na shetani kama wakala wake wa kumuangamiza Yusufu (Mwanzo 39:7-20)
(d). Yeyote au chochote kinachoharibu, kinachoiba yaliyomo ndani yako au kinachoua (Yohana 10:10)
-Kwa mfano mazungumzo mabaya yanayoharibu tabia njema (1 Wakorintho 15:33), madawa ya kulevya yanayoharibu na kuua vijana, marafiki wabaya nakadhalika.
(e). Chochote kinachokutenga na Mungu.
-Video au picha za ngono nakadhalika.
NB: Ninapofundisha kuhusu kumshinda shetani ni vema uwe ja picha kubwa ndani yako kuhusu shetani kama nilivyoeleza hapo kuhusu shetani ni nani ili ikusaidie kumjua adui huyo wa wanadamu.
VIJANA ALIOWAANDIKIA MTUME YOHANA
Vijana hao aliowaandikia mtume Yohana walimshinda shetani kutokana na mambo mawili
1. Walikuwa wamejaa neno la Mungu.
2. Walikuwa na nguvu za Mungu.
HITIMISHO
Kijana yeyote kama anataka kumshinda shetani lazima awe na nguvu za Mungu na neno la Mungu.
Hakikisha unasoma, kujifunza neno la Mungu na kuliishi, hakikisha unamtaka Mungu na nguvu zake kwa njia ya maombi.
0 Maoni