KUHUISHWA NA BWANA


(ZABURI 80:18)

Kuhuisha ni nini?

1. Ni kukipa kitu uhai.

2. Kukirejesha kitu katika hali yake ya kwanza.

Walipoomba kuhuishwa maana yake 

1. Walitambua hawako sawa ndio maana wakaombwa kuhuishwa.

2. Jambo  lililosababisha wakatambua hawako sawa ni kwa sababu walikuwa wamemwacha Mungu hawafuati sheria za Mungu pia walipoteza kiu ya kuomba ndio maana wakasema utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.

FAIDA ZA KUHUISHWA NA BWANA

1. Kiu ya maombi inaendelea kuongezeka ndani yako.

(Zaburi 80:18) wanasema wahuishwe ili WALIITIE JINA LA BWANA, Kuliitia jina la Bwana ni kuomba.

Kwa hiyo mtu akihuishwa na Bwana anakuwa na mzigo na kiu ya kuomba.


2. Inakuwa rahisi kuongozwa na Bwana.

(Zaburi 23:3)

UTAJUAJE UMEHUISHWA NA BWANA?

1. Angalia kama unafuata sheria au neno la Mungu.

2. Angalia kama una kiu na mzigo wa kuomba.


Ukiona haufuati neno la Mungu, umepoteza kiu na mzigo wa kumuomba Mungu, umekata tamaa, umeacha kumtumikia Mungu, OMBA MUNGU AKUHUISHE.


Chapisha Maoni

0 Maoni