Tunaposoma Biblia tunaona kuna makundi (timu) yamewahi kuundwa kwa ajili ya kazi mbalimbali.
Kwa mfano:-
●Mungu alimwambia Musa aunde timu ya watu kumi na mbili kwa ajili ya kuipeleleza nchi ya Kanaani (Hesabu 13:1-3)
●Yoshua aliunda kundi la watu wawili ili kwenda Yeriko kufanya upelelezi (Yoshua 2:1).
●Bwana Yesu aliunda timu ya watu sabini kisha akawagawa kwenye vikundi vidogo vidogo vya watu wawili kwa ajili ya utumishi (Luka 10:1,17-20).
●Yesu aliunda timu ya watu kumi na wawili aliowachagua akawaita mitume (Luka 6:13).
UUNDAJI WA VIKUNDI
●Kanisa linaweza kuunda vikundi mbalimbali kwa ajili ya utumishi.
●Watu binafsi wanaweza kuunda vikundi kwa ajili ya maombezi, timu kwa ajili ya ushuhudiaji, timu kwa ajili ya kumsifu na kumuabudu Mungu, timu kwa ajili ya kufanya usafi kwenye majengo ya kukutania kiibada, timu kwa ajili ya kupeleka injili kwa fedha zao, timukwa ajili ya kuelimisha jamii nakadhalika.
BAADHI YA MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA UUNDAJI WA VIKUNDI
●Ushiriki wa Mungu katika uundaji wa timu, ni vema Mungu naye apewe nafasi yake katika uundaji wa timu.
●Ni vema kuwepo na maono yaliyopelekea timu kuanzishwa ili iwe rahisi kuisimamia timu.
HITIMISHO
Kwa mujibu wa Biblia, uundaji wa vikundi (timu) limekuwa jambo mojawapo ambalo limechangia kufanikisha kazi mbalimbali za Mungu.
Hivyo basi taasisi au watu binafsi wanaweza kuunda timu kwa ajili ya utumishi wa namna mbalimbali.
0 Maoni