✍Faraja Gasto
Nakumbuka siku fulani nikiwa kwenye mkutano wa injili mahali fulani ghafla pepo wakaripuka tukaja pamoja kama waombaji.
Wakati tumekusanyika wengine wakaanza kuyauliza mapepo "jina lako nani" wakati huohuo sisi wengine tunawaamuru pepo watoke, ILICHUKUA MUDA KUWATOA WALE PEPO kwa kuwa walikuwa wanachanganywa.
Lakini Mungu alisaidia tukawatoa wale pepo.
NINACHOFUNDISHA NI KWAMBA
Wakati wa kutoa pepo ni vizuri kupatana kuyatoa kuliko kuyauliza mmetoka wapi, mliingiaje, mlitumwa na nani, mlikuwa mnakaa kwenye maini au figo au bandama, PEPO ANAPASWA KUTOLEWA TU MAANA YESU ALISEMA "TOENI PEPO" (MATHAYO 10:8)
Yamkini unaweza ukauliza mbona Yesu aliuliza pepo "jina lako nani" (MARKO 5:9)
Ukitazama andiko hilo utaona Yesu hakuwa na timu ya waombaji wakati anashughulikia hao pepo, Yesu alikuwa peke yake Biblia haijaeleza kwa undani kwa nini Yesu aliuliza pepo jina.
Hivyo basi naweza kufundisha kuwa mnapokuwa mnatoa pepo kama kundi au timu pataneni kwanza kulitoa pepo na si kuliuliza ila kama unatoa pepo mwenyewe na Roho anakuhimiza kumhoji pepo basi fanya kama Roho Mtakatifu anavyokuongoza.
0 Maoni