NGUVU YA UFUASI


 ✍Faraja Gasto

Yule unayemfuatilia sana au yale unayoyafuatilia sana YANA NGUVU YA KUKUATHIRI KATIKA NAMNA HASI AU CHANYA.

Ukiwa mfuatiliaji sana wa tamthilia zitakuathiri

Ukiwa mfuatiliaji sana wa mambo ya siasa yatakuathiri.

Chochote au yeyote unayemfuatilia ana nguvu ya kukuathiri.

MATHAYO 26:69-73

Mtume Petro alikuwa mfuasi wa Yesu, ilifika hatua ufuasi ulimuathiri hata kusema kwake.

●Kuna watu ukiwasikiliza leo unaweza kudhani Mwl. Mwakasege anaongea kumbe hapana.

●Kuna watu ukiwasikiliza unaweza kudhani ni Mzee Kulola anaongea kumbe hapana.

●Kuna watu ukiwasikiliza unaweza kudhani ni Renhard Bonke amefufuka kumbe hapana.

●Kuna watu tunasikia wanajitoa muhanga kwa kujilipua kwa mabomu ili wafe na watu fulani.

👆👆👆hiyo ni nguvu ya ufuasi.

IKO HIVI

Maisha yako, mienendo yako, usemi wako, mitazamo nakadhalika vinafunua unayemfuata au unachofuatilia.


NB: Kama wewe ni mfuasi wa Yesu, lazima kuna namna Yesu atakuathiri kabisa KWA NAMNA CHANYA.


👉Kama Yesu hajakuathiri basi fahamu kuwa bado haujawa mfuasi wa Yesu, siku ukiwa mfuasi wa Yesu tutajua tu hakuna haja ya kujitangaza kwamba umeokoka unampenda sana Yesu, tutajua tu.


Ukiwa mfuasi halisi wa Yesu hata ukikaa kimya watu watasema unaye Yesu, mienendo, usemi nakadhalika vitamfunua Yesu Kristo.


Nitaendelea ...............

Chapisha Maoni

0 Maoni