MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA IKIWA UNASONGWA NA MAMBO MENGI


 ✍Faraja Gasto

Kuna watu husema tunashindwa kuomba kwa kuwa tumesongwa na mambo mengi (we're so busy).

Yesu alikuwa ana majukumu mengi lakini aliomba (alikuwa mwombaji).

Baadhi ya mbinu za kukusaidia kuomba ikiwa umesongwa na mambo mengi.

●Amka alfajiri mapema anza kuomba.

(Marko 1:35) Yesu aliitumia mbinu hii.

-Omba kabla haujaanza kutekeleza majukumu yako.

●Omba ukiwa unatembea (prayer walking), kama unakwenda sehemu fulani kwa miguu, tumia muda huo kuomba ukiwa unatembea.

●Ukiwa chooni, bafuni omba, Mungu hazuii mtu kuomba akiwa popote pale.

-Yona aliomba akiwa ndani ya tumbo la samaki.

●Tumia sehemu ya muda wa mapumziko, chai au chakula kumuomba Mungu kwa ajili ya mambo mbalimbali.

-Kuna wengine kazini kwao huwa kuna vipindi vya mapumziko, chai na chakula, tumia sehemu ya muda huo kuomba.

Chapisha Maoni

0 Maoni