NGUVU YA UFUASI - 2

✍Faraja Gasto

Katika sehemu ya kwanza nilifundisha kwamba chochote au yeyote unayemfuatilia ana nguvu ya kukuathiri kwa namna chanya au hasi.

Katika sehemu hii ya pili nataka kufundisha kuhusu UFUASI KAMA MLANGO WA ROHO KUTOKA MBINGUNI AU KUZIMU.

Nikupe shuhuda chache kuhusu namna ufuasi unavyosababisha roho fulani kuwaingia watu;-

●Kuna watu wamejiua kwa sababu timu za mpira wanazoshabikia zimefungwa, roho ya kujiua zinaingia kutokana na ufuasi wao.

●Kijana fulani alipokuwa kwenye ukumbi wa maonyesho ya mechi za mpira wa miguu, timu aliyokuwa anashabikia ilipofungwa aliivunja ile runinga kwa kuwa timu aliyokuwa anashabikia imefungwa, hiyo ni roho kutoka kuzimu iliyomuhimiza kuvunja runinga.

Kama wewe sio mfuasi wa timu za mpira wa miguu utasema hao wanaojiua au kufanya mambo mabaya kwa kuwa timu zao zimefungwa hawana akili, ila unapaswa kufahamu kuwa UFUASI NI MLANGO WA ROHO KUTOKA KUZIMU AU MBINGUNI.

Hao hufanya matukio hayo kwa kuwa kuna roho huwaingia na kuwasukuma kutenda mambo hayo (kujiua na kufanya mambo mabaya), mlango iliopitia ni ufuasi.

(Matendo ya mitume 2:1)

Biblia inaripoti kuwa Roho Mtakatifu aliwashukia wafuasi wa Yesu, ukitazama utaona Roho hakushuka kwa kila mtu bali kwa wafuasi wa Yesu Kristo.

Kilichosababisha Roho Mtakatifu awashukie hao ni kwa sababu walikuwa wafuasi wa Yesu kwa hiyo Roho wa Yesu akawaingia.

IKO HIVI

Kila jambo hapa duniani lina roho nyuma yake au lina roho ndani yake.

Kuna watu wameingiwa na roho za uzinzi na ukahaba baada ya kuanza kufuatilia tamthilia au filamu fulani hususani filamu na tamthilia za mambo ya ngono.

Kuna watu wameingiwa na roho za mauti baada ya kuanza kuwa wafuatiliaji wa filamu fulani, hatimaye wakaona kujiua sio vibaya ni kuepuka matatizo au kuua wengine sio vibaya.

Kuna watu wameingiwa na roho za uasi na roho zidanganyazo baada kuanza kufuatilia mafundisho au elimu fulani.

NAMNA YA KUISHINDA ROHO ILIYOKUINGIA KUTOKA KUZIMU KUTOKANA NA KUFUATILIA MAMBO FULANI

●Kama haujamwamini Yesu, mwamini Yesu.

●Acha kufuatilia mambo hayo yaliyosababisha roho hiyo au roho hizo zikakuingia.

●Weka neno la Mungu kwa wingi ndani yako, neno la Mungu ni upanga wa Roho mtakatifu (Waefeso 6:17)

Nitaendelea.........

Chapisha Maoni

0 Maoni