NGUVU YA UFUASI - 3 MWISHO

✍Faraja Gasto

 

Katika sehemu ya pili nilifundisha ufuasi kama mlango wa kuingiza roho kutoka mbinguni au kuzimu .

Katika sehemu hii ya tatu nataka kufundisha kuhusu NAMNA YA KUMFUATA YESU.

Yesu alitoa miongozo kuhusu namna ya kumfuata yeye, alisema hivi ukitaka kumfuata.

●Jikane na ujitwike msalaba wako kila siku (Luka 9:23)

Ufafanuzi ambao ni rahisi kuuelewa kuhusu kujikana na kubeba msalaba ni kwamba "uwe tayari kulipa gharama za kumfuata Yesu kila siku" kwa kuwa kuna gharama za kumfuata utapaswa kulipa.

Mfano, Yesu aliwaambia wakina Petro wamfuate yaani waache kazi zao wamfuate yeye, kumfuata Yesu kuliwaachisha kazi.

Hata injili iliyotufikia huku Afrika iliwagharimu wengine, wengine waliuawa kwenye harakati za kupeleka injili, wengine waliteswa sana hatimaye injili ikatufikia huku Afrika.

●Jifunze kwa Yesu (uwe mwanafunzi kila siku) (Mathayo 11:29)

Huwezi kuwa mfuasi kama haujifunzi kwake ndio maana aligiza watu wafanywe wanafunzi (Mathayo 28:19-20)

Sisi ni wanafunzi tusiomaliza shule au chuo cha Yesu, kila siku ni siku ya kujifunza.

●Utii

(1 Samweli 15:11)

Mungu alisema Mfalme Sauli ameacha kumfuata kwa kuwa hakutii.

Yesu alipowaita watu wawe wafuasi walitii na kuanza kumfuata (Mathayo 4:20).

Kila ambacho Yesu anasema tunapaswa kukishika au kukitii (Mathayo 28:19-20)

Chapisha Maoni

0 Maoni