MIKONO KWA JINSI YA ROHONI


✍Faraja Gasto

Mambo tutakayojifunzakatika somo hili

☆Mambo baadhi ya kufahamu kuhusu mikono

☆Baadhi ya ishara zinazoonyesha mikono yako ina tatizo kiroho

☆Baadhi ya mbinu za kushughulikia mikono yako kwa jinsi ya rohoni.

MAMBO BAADHI YAKUFAHAMU KUHUSU MIKONO

●●Mikono inaweza kubeba mambo ya kiroho 

(Kumbukumbu la torati 34:9)(2 Timotheo 1:6)(Marko 16:8)(Mwanzo 39:3-4)

●●Kilichopo kwenye mkono au mikono yako kwenye ulimwengu wa roho kitadhihirika kwenye kazi zako kwenye ulimwengu wa mwili.

(Mwanzo 39:3-4)(2 Wafalme 5:1)

Kilichosababisha Mungu akakataa Mfalme Daudi asijenge hekalu ni kwa sababu ya mikono yake ilimwaga damu.

(1 Mambo ya nyakati 28:3) mikono ya Mfalme Daudi ilisababisha akakosa kibali cha kujenga hekalu. Kila mtu anapaswa kufahamu kuwa namna mikono yako ilivyo kwenye ulimwengu wa roho inaweza ikaathiri maisha yako kwenye ulimwengu wa kimwili.

●●Mikono yako inaweza kuwa sababu mojawapo ya Mungu kujibu au kutojibu maombi yako unayoyaomba.

(Isaya 1:15) Mungu aliwaambia wana wa Israeli hataki kujibu maombi yao kwa kuwa mikono yao ina tatizo kutokana na kumwaga damu.

(Zaburi 24:3-5) Mungu anasema jambo mojawapo linalosababisha mtu apokee Baraka kutoka kwake ni mikono yake iliyo safi, hazungumzii usafi unaotokana na kunawa au kuoga bali usafi wa mikono kwa namna ya rohoni.

BAADHI YA ISHARA ZINAZOONYESHA KUWA MIKONO YA MTU IMEPATA TATIZO KWA JINSI YA ROHONI 

●●Kuwashwa mikono au kusikia mikono inawasaha.

Watu wengi wanapoona mikono inawasha huwa wanasema ni dalili ya kupata fedha, wengine wanapoona hali hiyo huwa wanaandika kwenye mikono kiasi cha fedha wanachokitaka pasipo kujua suala la kuwashwa ni suala la kiroho. 

(Kumbukumbu la torati 28:22) Mungu anasema kuwashwa ni mojawapo ya pigo analowapiga watu ambao wamekataa kusikiliza na kufanya anachokisema, hilo linatupa kufahamu unapoona unawashwa hiyo ni dalili kuwa katika ulimwengu wa roho.

Mahali popote ambapo Mungu amezungumzia suala la kuwashwa basi ujue kuna tatizo Fulani kwa hiyo kuwashwa ni ishara mojawapo ya kimwili kutokana na jambo lililoendelea kwenye ulimwengu wa roho, soma (2 Wafalme 21:12)(1 Samweli 3:11)

●●Kuanza jambo halafu likaishia njiani au kuanza jambo halafu haulikamilishi.

(Zekaria 4:8-9) Zerubabeli alianza ujenzi lakini hakuukamilisha kutokana na jambo lililotokea kwenye ulimwengu wa roho likaathiri mikono yake ndio maana Mungu alipoingilia kati jambo mojawapo aliloshughulikia ni mikono ya Zerubabeli ndio maana Mungu alisema “mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii na mikono yake ndiyo itakayoimaliza” (Zekaria 4:9)

●●Kufanya kazi halafu haunufaiki na kazi za mikono yako.

Kufanya kazi halafu haunufaiki na kazi za mikono yako ni ishara mojawapo inayoonyesha kuwa kuna jambo haliko.

Mapenzi ya Mungu ni kuona unanufaika na kazi za mikono yako (Isaya 65:22)

●●Uwepo wa vikwazo vinavyokuzuia kutekeleza wazo zuri ulilonalo moyoni mwako.

(1 Mambo ya nyakati 28:3) Mfalme Daudi alikuwa na wazo la kumjenegea Mungu hekalu lakini Mungu alikataa kwa kuwa mikono yake ilikuwa imetumika kumwaga damu nyingi za watu.

Mikono yake ilikuwa kikwazo kwa wazo alilokuwa nalo moyoni mwake.

BAADHI YA MBINU ZA KUSHUGHULIKIA MIKONO YAKO KWA JINSI YA ROHONI

●●Safisha au nawa au takasa mikono yako kwa damu ya Yesu.

(Zaburi 24:3-4) Biblia imezungumza kuhusu usafi wa mikono, hiyo ni sawa na kusema kwamba mikono inaweza kuchafuka kwa jinsi ya rohoni. Ili mikono iwe safi kwa jinsi ya rohoni ni vema itakaswe kwa damu ya Yesu.

●●Ifungue mikono yako.

Maaskari wanapomkamata mtu kuna wakati huwa wanafunga mikono yake, vivyo hivyo katika ulimwengu wa roho mikono ya mtu inaweza kufungwa.

Katika hali ya kawaida mikono ikifungwa hauwezi kupigana, hauwezi kufanya kazi nakadhalika vivyo hivyo katika ulimwengu wa roho mikono ikifungwa mtu atajikuta amepata shida mbalimbali kwenye ulimwengu wa mwili.

(Waamuzi 15:13-14) watu walimfunga mikono Samsoni ili asifanye jambo lolote, Roho wa Mungu aliposhuka juu yake alimuwezesha kukata zile kamba zilizotumika kufunga mikono yake.

Vivyo hivyo katika ulimwengu wa roho zipo kamba na minyororo inayotumiwa kufunga mikono ya watu, ili mikono iwe huru kata hizo kamba au vunja kamba au minyororo iliyofunga mikono yako kwenye ulimwengu wa roho.

●●Rejesha vilivyochukuliwa kutoka mikononi mwako.

(Ufunuo 3:11) ulichonacho mikononi kwenye ulimwengu wa roho kinaweza kuchukuliwa usipokuwa makini, hivyo basi rejesha kilichoibiwa au kuchukuliwa kutoka kwenye mikono yako kwenye ulimwengu wa roho.

Chapisha Maoni

0 Maoni