MTU WA WATU


 ✍Faraja Gasto

Sifa mojawapo ya kiongozi bora kwa mujibu wa Biblia ni "mtu wa watu" yaani kiongozi bora ni mtu wa watu (1 Wafalme 12:7)

Mtu wa watu ni mtu asiyeumiza watu, asiyebagua watu, haonei watu, asiyependelea watu, hafanyi mambo kwa maslahi yake binafsi au maslahi ya watu fulani tu, ni mtu anayesikiliza na kuzingatia maoni ya watu ambayo hayako kinyume na mapenzi ya Mungu, anajali watu nakadhalika.

Kama unaongoza watu unapaswa kuwa mtu wa watu, ikiwa unataka kuwa kiongozi halafu umeshindwa kuwa mtu wa watu basi fahamu kuwa UONGOZI UMEKUSHINDA KABLA HAUJAANZA KUONGOZA na ikiwa unaongoza watu ilihali wewe sio mtu wa watu basi fahamu kuwa UONGOZI UMEKUSHINDA.

NB: Kujitahidi kuongoza wakati uongozi umekushinda ni kujitesa mwenyewe na kuwatesa wengine.

Chapisha Maoni

0 Maoni