Kaini na Habili walitoa sadaka sio kwa sababu walitaka wabarikiwe.
Nuhu alitoa sadaka sio kwa sababu alitaka abarikiwe.
Baba yetu Ibrahimu alitoa sadaka sio kwa sababu alitaka abarikiwe.
Mungu hakumtoa mwanawe wa pekee ili abarikiwe bali arejeshe na kuendeleza mahusiano na wanadamu.
NB:
●Ni ukweli usiopingika kuna baraka zinazotokana na utoaji wa sadaka ila ukiona unatoa sadaka ili Mungu akubariki basi fahamu kuwa ufahamu wako una hitilafu kidogo katika eneo la sadaka.
●Baada ya kufahamu lengo la awali la utoaji wa sadaka itakusaidia kufahamu kuwa "Mungu haiishii kutaka sadaka ila anataka na moyo wa mtoa sadaka" anataka mtoa sadaka awe na mahusiano mazuri na yeye.
0 Maoni