(LUKA 1:1-4)
Luka alikuwa Daktari kitaaluma, hakuwa mtume kati ya wale mitume kumi na mbili wa Kristo Yesu lakini mbali na taaluma yake alimtumikia Mungu kwa njia mbalimbali ikiwemo uandishi.
Huyu ndiye mwandishi wa kitabu cha Luka kilichomo ndani ya Biblia kwenye orodha ya vitabu viitwavyo agano jipya, aliandika kitabu hicho kumuelimisha Mhe. Theofilo lakini kitabu hicho kimefanyika baraka hata kwetu sisi tusiofahamiana na Mhe. Theofilo.
IKO HIVI: Uandishi ni kazi mojawapo ambayo unaweza kumtumikia Mungu kwayo.
Usiseme mimi sio mtume, Nabii, mwalimu, mwinjilisti na mchungaji, usiseme mimi sijaitwa na Mungu,TAFUTA KAZI YA KUFANYA KAMA UTUMISHI KWA MUNGU.
Luka anatujulisha kuwa hakufunuliwa aliyoyaandika bali ALIJITAFUTIA USAHIHI WA MAMBO KISHA AKAANDIKA ALIYOYAANDIKA.
Mambo ya kuandika ni mengi sana, kama una kiu ya kumtumikia Mungu kupitia uandishi, haya ni baadhi ya mambo ya kuandika ili watu wajifunze;-
●Andika kuhusu wadudu, wanyama, miti nakadhalika yapo ambayo tunaweza kujifunza kupitia wadudu, wanyama, miti nakadhalika si unajua Biblia imemshauri mvivu ajifunze kwa mdudu aitwaye chungu (Mithali 6:6), si unajua Yesu alisema kwa mtini jifunzeni (Mathayo 24:32).
●Andika historia za watu, tawala, maeneo nakadhalika.
(Kutoka 17:14) Mungu alimwambia Musa aandike kitabu kuhusu historia ya vita vya Waisrael na Waamaleki iwe ukumbusho.
0 Maoni