✍Faraja Gasto
●SIKILIZA NA UPOKEE MAONO YA VIJANA.
Vijana wanayo maono ya aina mbalimbali, ni muhimu kuwasikiliza.
(2 Wafalme 6:1)
Nabii Elisha alisikiliza maono ya vijana na akayapokea.
Kama wewe ni kiongozi wa huduma au taasisi ni vema uwe na utaratibu wa kuwasikiliza vijana wana maono gani.
●YAUNGE MKONO MAONO YA VIJANA.
(2 Wafalme 6:2-4)
Baada ya Nabii Elisha kusikiliza na kupokea maono ya vijana aliwaunga mkono ndio maana alipoombwa na yeye ashiriki maono hayo alikubali.
●SHIRIKI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOKWAMISHA MAONO YA VIJANA.
(2 Wafalme 6:4-7)
Katika harakati za kutimiza maono yao hao vijana, mmoja wao aliangusha shoka aliyoazima akamjulisha Nabii Elisha, Nabii Elisha alishiriki kutatua changamoto ile hatimaye maono ya vijana wale yakatimia (wakapata miti ya kujengea)
●WAAMINI VIJANA NA UWAPE NAFASI YA KUDHIHIRISHA UWEZO WAO AU VILIVYOMO NDANI YAO.
(1 Samweli 17:32-55)
Daudi alipomwambia Mfalme Sauli kwamba "ninaweza kumuua Goliathi" Mfalme Sauli hakuamini lakini aliamua kumpa nafasi ya kupigana na Goliathi hatimaye Daudi alimuua Goliathi.
●WAFUNDISHE VIJANA KUPIGANA VITA NA UWAPELEKE VIJANA VITANI.
(Hesabu 1:1-3)
Mungu alimwambia Musa awahesabu wana wa Israeli ikiwa ni pamoja na vijana wenye umri kuanzia miaka ishirini ambao wanaweza kwenda vitani.
Ni kweli katika agano jipya hatufanyi vita kwa jinsi ya mwilini bali kwa jinsi ya rohoni ila vijana wengi hawajui vita kwa kuwa hawajafundishwa na hawajapelekwa vitani.
Kwa mfano kuna mahali unakuta mchungaji anakemea pepo halafu vijana wamemshika mwenye pepo, vijana waliolelewa hivyo wakiona mtu mtu ana pepo hawatashughulika naye bali watamuita mchungaji aje kushughulikia pepo.
Ni vizuri kuwafundisha vijana vita za aina mbalimbali halafu wakati mwingine wapeleke vitani wakapigane.
0 Maoni