Kaini alipomuua ndugu yake yaani Habili alidhani amemuweza kumbe alikuwa amejizalishia balaa kwenye maisha yake.
IKO HIVI unaweza kuua mtu lakini hauwezi kuua damu yake, damu yake itakutesa itakusababishia majanga makubwa.
Mwanzo 4:10-11
(Mungu) Akasema, Umefanya nini? SAUTI YA DAMU ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako.
NB: Usiue kwa namna yoyote (kutoa mimba, kuchinja mtu, kupiga mtu risasi n.k) ukiua mtu damu yake itakusababishia majanga makubwa.
0 Maoni