LAANA


 ✍✍Faraja Gasto

Laana ni kitu kimojawapo kinachotesa maisha ya watu wengi na maeneo mengi sana hapa duniani, zipo aina nyingi sana za laana kwa mfano laana ya kuwa mtumwa wa wengine (Mwanzo 9:24-25), laana ya kutangatanga (Mwanzo 4:10-11), laana za magonjwa (Kumbukumbu la torati 28:21-22) kuna familia au ukoo ambao watu wa ukoo huo wana magonjwa ya kufanana kama ni presha utaona babu alikuwa na presha, baba ana presha, watoto wana presha, na zingine nyingi, soma (Kumbukumbu la torati 28:15-68)(Zaburi 109:6-20)

Kiumbe cha kwanza kulaaniwa ni nyoka (Mwanzo 3:14) laana ilibadilisha kabisa maisha ya nyoka.

Laana zina nguvu ya kuharibu maisha ya watu, kumdhoofisha mtu na kumfungulia shetani milango ya kufanya kazi zake kwenye maisha ya mtu au watu. Yesu aliulaani mti ukakauka (Mathayo 21:18-19), Laana zinaweza kufuatilia watu kizazi kimoja hadi vizazi vingine.

BAADHI YA MAKUNDI YA LAANA

1. Laana zinazotokana na kutokutoa fungu la kumi (Malaki 3:9-10)

2. Laana zinazotokana na wazazi, wazazi wako hata kama hawajaokoka wana mamlaka kwenye ulimwengu wa roho ya kufungulia mambo mabaya kwako, Nuhu alikuwa mlevi lakini alitamka laana na ikashika (Mwanzo 9:24-25) Wakanaani walitolewa kwenye nchi yao wakapewa waisraeli kwa kuwa laana ilikuwa juu yao.

3. Laana zinazotokana na kuwategemea wanadamu (Yeremia 17:5) ukiwategemea wanadamu unafungulia laana kwenye maisha yako.

4. Laana zilizopo kwenye mazingira fulani (Yoshua 6:26)(1 Wafalme 16:34) Yoshua alitamka laana impate mtu yeyote atakayejenga tena mji wa Yeriko ile laana ilikaa pale Yeriko alipotokea mtu wa kujenga Yeriko ile laana ilimpata (1 Wafalme 16:34) 

5. Laana zinazotokana na kuua mtu au kumwaga damu ya mtu (Mwanzo 4:10-11) unaweza kuua mtu lakini hauwezi kuua damu ya mtu, damu ya mtu huwa haifi (Mwanzo 4:10-11)

6. Laana zinazotokana na kutokumtii na kumtumikia Mungu (Kumbukumbu la torati 28:15-68)

7. Laana zinazotokana na kuwainukia watumishi wa Mungu (kuwasema vibaya watumishi wa Mungu, kuwadhuru watumishi wa Mungu n.k) (Zaburi 109)

LAANA KAMA SILAHA

Laana ni mojawapo ya silaha ambayo Mungu huitumia na shetani huitumia, pia wapo watu mbalimbali ambao walitumia laana 

1. Wamoabi kabla hawajapigana na waisraeli walifanya mpango wa kuwalaani (Hesabu 22:1-7) walitaka wawalaani kwa kuwa walijua laana zina nguvu ya kumdhoofisha mtu, kuharibu maisha ya mtu nakadhalika.

2. Goliathi kabla hajapigana na Daudi alimlaani kwanza ili kumdhoofisha (1 Samweli 17:43)

3. Nabii Elisha aliwalaani vijana hatimaye walikufa (2 Wafalme 2:25)

BAADHI YA MBINU ZA KIBIBLIA ZA KUKABILIANA NA LAANA MBALIMBALI

1. Omba Mungu akusamehe kwa kutokumtii na kutokumtumikia kwa kuwa hiyo ni sababu mojawapo inayofungulia laana kwenye maisha ya mtu (Kumbukumbu la torati 28: 15-68)

2. Omba Msamaha kwa mtu uliyemkosea aliyekutamkia laana, kwa mfano kama umetamkiwa laana na wazazi au mzazi (Mwanzo 9:24-25) Nuhu alitamka laana lakini mtoto wake hakuomba msamaha kwa kosa lake na kwa kuwa hakuomba msamaha ile laana ikamshika Kanaani na uzao wake.

3. Tumia damu ya Yesu kufuta na kuvunja laana mbalimbali (ulizotamkiwa au zilizoandikwa Hesabu 5:23) kwa kuwa damu ya Yesu ina nguvu ya kufuta na kuvunja laana (Wagalatia 3:13)

4. Toa fungu la kumi, Mungu aliwaambia waisraeli wamelaaniwa kwa kuwa Hawatoi fungu la kumi (Malaki 3:9-10) kwa hiyo ili laana iwaachie walipaswa kutoa zaka.

5. Unaponunua uwanja au unapotaka kujenga nyumba hakikisha unafanya maombi kabla haujajenga kwenye kiwanja ulichonunua, kabla haujaenda kupanga kwenye nyumba au kama umepanga kwenye nyumba fulani hakikisha unaombea eneo la nyumba hiyo ili kama kuna kitu kibaya hapo Mungu akishughulikie. (Yoshua 6:26) Yoshua aliacha laana kwenye mji wa Yeriko alipoinuka mtu wa kujenga mhi wa Yeriko alifiwa watoto wawili (1 Wafalme 16:34) laana ya Yoshua ilimpata.

Chapisha Maoni

0 Maoni