(Isaya 46:9)
UTANGULIZI
Mojawapo ya jambo ambalo Mungu aliwaambia wana wa Israeli ni hili “wasimsahau yeye baada ya kufanikiwa” (Kumbukumbu la torati 8:11-20)
Watu wengi wanapofanikiwa humsahau Mungu kabisa, husahau kule Mungu alipowatoa (Yeremia 22:21)
Mojawapo ya tatizo walilokuwa nalo wana wa Israeli ilikuwa ni kusahau kule Mungu alikowatoa, (Kutoka 20:1) Mungu aliwaambia ni yeye aliyewatoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa.
KWA NINI MUNGU ANATAKA UKUMBUKE ALIKOKUTOA
a). Ili uzidi kumtegemea yeye.
(Zaburi 124) Hiyo zaburi haiwezi kuwa na maana kwa mtu aliyesahau kule Mungu alikomtoa, ukikumbuka Mungu alipokutoa utaendelea kumtegema kwa kuwa utakuwa unafahamu bila Mungu hauwezi lolote, kama ulifanikiwa sio kwa nguvu zako bali Mungu alikupa nguvu zake (Kumbukumbu la torati 8:11-20)
b). Kukumbuka kule Mungu alipokutoa kutakufanya uendelee kumpa Mungu heshima yake na nafasi anayostahili kwenye maisha yako.
(Zaburi 124) neno “kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi” limerudiwa mara nyingi kuonyesha kuwa ni Mungu tu aliyewatendea mambo yote mema na kwa kuwa ni MUNGU aliyetenda basi anastahili heshima na nafasi ya kwanza kwao.
c). Kukumbuka Mungu alipokutoa kunarejesha matumaini ndani yako na kukupa nguvu mpya.
(1 Samweli 17:32-37) jambo lililompa nguvu Daudi kwenda kumkabili Goliathi ni kumbukumbu, alikumbuka jinsi Mungu alivyomsaidia kuua samba na dubu akaona kama Mungu alimsaidia kuua samba na dubu basi atamsaidia kumuua Goliathi.
Na wewe kumbuka Mungu alipokutoa, kama alikupitisha mahali pagumu anaweza kukupitisha mahali pagumu endapo utapita mahali pagumu.
0 Maoni