Sehemu tatu za somo
· Aina za sadaka
· Aina za utoaji wa sadaka ambao Mungu anaupenda
· Mambo ya kuzingatia kabla haujatoa sadaka
AINA ZA SADAKA
ü Malimbuko (Mithali 3:9)
ü Zaka (Malaki 3:10)
ü Sadaka za shukrani (Zaburi 50:23)
ü Sadaka za kuwapa watu (Matendo ya mitume 10:1-2)
ü Sadaka ya kushirikiana na wengine (Waebrania 13:16) kwa mfano (Matendo ya mitume 4:32) watu walikuwa na vitu vyote shirika yaani kile walichokuwa nacho kilikuwa si kwa ajili yao tu bali kwa ajili ya wengine
ü Kuwatendea watu mema (Waebrania 13:16)
ü Sadaka za ibada (1 Wafalme 3:4) ni sadaka ambazo watu hutoa kama sehemu ya ibada kila wanapokusnyika mbele za Mungu.
ü Sadaka za utumishi, kwa mfano kuwaombea watumishi wa Mungu, kutoa sadaka ili kupeleka injili nakadhalika.
AINA ZA UTOAJI AMBAZO MUNGU ANAZIPENDA
o Kutoa kwa moyo wa kupenda (2 Wakorintho 9:7)
o Kutoa kwa imani (Waebrania 11:4) imani chanzo chake ni kusikia (Warumi 10:17) kutoa kwa imani ni kutoa sadaka baada ya kusikia Mungu akikupa maelekezo ya kutoa, utoe nini, utoe lini, utoe wapi, utoe kwa kiwango gani nakadhalika.
0 Maoni