MAMBO AMBAYO KILA KIONGOZI WA NCHI ANAPASWA KUYAFAHAMU

 

1.    Nchi ni mali ya Mungu kwa kuwa yeye ndiye aliyeumba mbingu nan chi (Mwanzo 1:1)(Zaburi 24:1)

2.    Mungu analo neno kwa ajili ya kila nchi kutegemeana na nyakati mbalimbali (Mwanzo 41:56-57)

3.    Nchi ni kama viungo vya mwili, hivyo basi kila nchi ni muhimu kwa nchi zingine, nchi moja ikiathirika basin chi zingine zitaathirika kwa namna mbalimbali , hivyo basin chi inapaswa kufanyika Baraka kwa nchi zingine (Mwanzo 41:56-57)

4.    Mungu ana suluhisho la matatizo yote ya nchi endapo atapewa nafasi ya kutatua matatizo hayo (2 Samweli 21:1-9)

5.    Mungu humpa mtu au huwapa watu nchi (Mwanzo 28:13)(Mwanzo 12:7) hivyo basi suala la kutawala nchi ni suala la kiroho kabla halijawa kimwili, nchi inatawaliwa kiroho na kimwili. Ili mtu atawale nchi vizuri lazima ajiambatanishe na Mungu ambaye mbingu nan chi ni mali yake.

6.    Kiongozi wan chi sio tu mwanasiasa bali wakili wa Mungu katika nchi, wakili wa Mungu humwakilisha Mungu katika nchi, kumwakilisha Mungu maana yake ni kufanya jambo Fulani kwa niaba ya Mungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni