(Mathayo 1:18-21)
Mambo utakayojifunza
1.Kusudi la kuzaliwa kwa Yesu
2.Namna tunavyopswa kusherehekea sikukuu ya
kuzaliwa kwa Yesu
UTANGULIZI
Watu wengi wakristo na wasio wakristo
wamekuwa wakifanya sherehe katika sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu maarufu kama
krismasi (Christmass).
Watu wengi wakristo na wasio wakristo
wamekuwa wakisherehekea vibaya sikukuu hii kutokana na kutofahamu hasa lengo la
kuzaliwa kwa Yesu au lengo la Yesu kuja hapa ulimwenguni.
Watu wengi wamekuwa wakiweka nguvu nyingi
katika manunuzi ya vitu mbalimbali kama mavazi na chakula pamoja na kwenda kutalii sehemu mbalimbali,
sio vibaya kufanya hayo yote nyakati za sherehe ila kabla ya kuwekeza nguvu
nyingi katika mambo hayo ni vema uwe na ufahamu kuhusu sherehe hii kiini chake
ni nini, ukifahamu lengo la Yesu kuja hapa duniani naamini hautasherehekea
kimakosa.
N.B Tunaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu tarehe
25 mwezi wa 12 kila mwaka haimaanishi kuwa Yesu alizaliwa tarehe hiyo ila
tunaitumia siku hiyo kukumbuka au kama kumbukumbu ya upendo wa Mungu kwa
wanadamu kwa kumtoa mwanawe wa pekee kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu.
KUSUDI LA
KUZALIWA KWA YESU
(Mathayo 1:21)
“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na
dhambi zao.”
Kutokana
na andiko hilo tunapata kufahamu kuwa kusudi la Yesu kuja hapa ulimwenguni ni
ili “AWAOKOE WATU WAKE NA DHAMBI ZAO”
(Luka
10:19)
“Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile
kilichopotea.”
Kutokana
na fungu hilo tunapata kufahamu kuwa Yesu “ALIKUJA KUTAFUTA NA KUOKOA KILE
KILICHOPOTEA”
Kwa
kuwa Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea ndio maana malaika wa
Mungu wanasherehekea pale mwenye dhambi mmoja anapotubu au anapomwamini Yesu.
“Nawaambia, Vivyo hivyo
kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko
kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.”
(Luka 15:7)
NAMNA TUNAVYPASWA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KUZALIWA KWA
YESU (CHRISTMASS)
1.
Tunapaswa kuwaambia wengine habari za Yesu ili waokoke
(tunapaswa kuhubiri injili)
(Mathayo 28:19-20)
“19. Basi, enendeni,
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana,
na Roho Mtakatifu; 20. na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na
tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
Kwa
kuwa kusudi la kuzaliwa kwa Yesu ni kuwaokoa wanadamu, tunapaswa kusherehekea
sikukuu hii kwa kuwashuhudia wengine au kuwaambia wengine habari za Yesu au
kuhubiri injili.
2.
Tunapaswa kutoa fedha zetu au vifaa mbalimbali
vitakavyosababisha injili iwafikie wale ambao hawajamwamini Yesu.
(Warumi
10:14-15)
“14. Basi wamwiteje yeye
wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye
wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo
mhubiri? 15. Tena wahubirije,
wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio
habari ya mema!”
Sisi
ambao tayari tumemwamini Yesu tunapaswa kutoa fedha zetu ili injili ihubiriwe,
tunapaswa kununua vifaa vya kuhubiria injili na kuwapa wahubiri au kuvitoa
makanisani ili injili izidi kuhubiriwa pia tunapaswa kuwasafirisha wahubiri wa
injili ili waende kwenye umisheni.
Biblia
imeweka wazi kuwa hakuna askari aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe,
askari anahitaji kupelekwa.
“Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama
zake mwenyewe?” (1 Wakoritho 9:7a)
3.
Tunapaswa kumpa Mungu vilivyo bora .
(Mathayo
2:11)
Mamajusi
walipokuja kumtazama Yesu walimtolea Yesu tunu, uvumba, dhahabu na manemane.
Tunaposherehekea
kuzaliwa kwa Yesu tunapswa kukumbuka kuwa Yesu alitolewa na Mungu kama zawadi
ya Mungu kwa ulimwengu ili wanadamu waokolewe, kama Mungu alitoa kilicho bora
na cha thamani (mwanawe wa pekee) nasi tunapaswa kumpa Mungu ambavyo ni bora na
vya thamani.
5 Maoni
Tunashukuru Sana kwa somo joli ambalo linatukumbusha tena namna ya kusherekeya kuzaliwa kwa Yesu Mungu awabariki
JibuFutaAmen
FutaNimebalikiwa na somo Hilo nawe ubarkiwe
JibuFutaMay God blesses you
JibuFutaAmen
Futa