Yapo matatizo mbalimbali ya uzazi yanayowasumbua wanaume na wanawake, tatizo mojawapo la uzazi kwa wanawake ni kukosa uwezo wa kubeba mimba.
Kwa mujibu wa Biblia, sababu mojawapo inayosababisha wanawake kutokubeba mimba ni KUFUNGWA KWA TUMBO LA UZAZI LA MWANAMKE KWA JINSI YA ROHONI, soma (Mwanzo 20:18)(Mwanzo 16:2)(1 Samweli 1:5-6).
MAMBO BAADHI UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU TUMBO LA UZAZI LA MWANAMKE
1. Tumbo la uzazi la mwanamke linaweza kufungwa au kufunguliwa kwa jinsi ya rohoni, tumbo linaweza kufungwa na nguvu za giza au Mungu mwenyewe, soma (Mwanzo 30:22)(Mwanzo 29:31)(Mwanzo 20:18)(Mwanzo 16:2)(1 Samweli 1:5-6).
2. Huwezi kuzaa ikiwa tumbo lako la uzazi limefungwa, ili uweze kuzaa lazima tumbo lako la uzazi lifunguliwe, soma (Mwanzo 30:22)(Mwanzo 29:31)
NAMNA YA KUOMBEA TUMBO LA UZAZI LA MWANAMKE
1. Omba Mungu asamehe dhambi au uovu uliosababisha tumbo la uzazi likafungwa, soma (Mwanzo 20:17-18).
Mfalme Abimeleki alipomchukua Sara ili awe mkewe, Mungu aliyafunga matumbo ya watu wa nyumbani kwa Abimeleki kwa kuwa Abimeleki alichukua mke wa mtu (mke wa Ibrahimu), Mungu aliposamehe, wanawake walifunguliwa matumbo yao wakazaa.
2. Kemea nguvu za giza ambazo zimefunga tumbo la uzazi ili mwanamke asizae, kumbuka nimekufundisha kuwa nguvu za giza zinaweza kufunga tumbo la mwanamke asizae, zikikemewa zikatoka, mwanamke anaweza kuzaa.

0 Maoni