Ukweli ni kwamba kuna matatizo mengine huwa tunasababishiwa na watu wengine kwa mfano kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi (Warumi 5:22).
Usisahau kujitafakari, je! wewe ni msababisha matatizo kwa wengine au msababisha mema kwa wengine!!
Usisahau kuwaombea wengine kwa kuwa Mungu na shetani hutumia wengine kufanya mambo mbalimbali kwenye maisha yako.
Pia usisahau kuwa Mungu hutubariki sio kwa ajili yetu tu bali kwa ajili ya wengine.

0 Maoni