(Isaya
43:4)
Unaposoma andiko hilo
utaona Mungu anasema atatoa watu kwa ajili yako na kabila za watu kwa ajili ya
maisha yako ila amesema na sababu itakayomfanya atoe watu kwa ajili yako ni
“THAMANI” kwa hiyo kwa andiko hilo tunapata kujua kuwa thamani uliyonayo kwa
Mungu ndio inamfanya Mungu akuinulie watu wa kusimama na wewe katika maeneo
mbalimbali, kumbuka kama wewe ni mfanyabiashara unahitaji watu(wateja), kama
wewe ni Mchungaji unahitaji watu(washirika) kwa hiyo kila mtu kuna aina ya watu
anaowahitaji kulingana na mazingira fulani.
SWALI: Je! una thamani
kiasi gani mbele za Mungu?
Kila mwanadamu anapendwa
na Mungu na kila mwanadamu ana thamani mbele za Mungu lakini thamani inazidiana
kati ya mtu na mtu na hata upendo wa Mungu juu ya watu huwa unatofautiana kati
ya mtu na mtu na ukitaka kuamini hili soma biblia yako kwenye kitabu cha (Danieli
10:11) utaona Danieli sanaambiwa kuwa yeye ni mtu apendwaye sana. Nikupe
mfano huu juu ya thamani, ninajua una nguo tofautitofauti na katika nguo hizo
kuna nguo ambazo unazipenda sana kuliko zingine na si ajabu hata zikichafuka
huwa unazifua kwa kutumia sabuni ya unga na sio sabuni ya mche, na si ajabu hata
ukizianika nguo hizo huwa unaweka na vibanio ili zisianguke chini kwenye
uchafu, na si ajabu unapozivaa huwa unabadilisha na muondoko, na si ajabu
unapozivaa nguo hizo huwa hupendi kuguswaguswa na nina uhakika huwa hauzivai
mara kwa mara na nina huwa kuna siku maalumu za kuvaa nguo hizo kutegemeana na
mahali unapokwenda na nina uhakika huwa ukizifua hizo nguo huwa unaziweka ndani
ya begi, Lakini kuna nguo ambazo huwa unashindia au huwa unazivaa ukiwa upo
nyumbani. Kinachokufanya ufanye mambo hayo yote ni kitu kinachoitwa “THAMANI”
thamani ya nguo ndio inaipa nguo heshima na inaifanya ngu ipendwe kuliko
zingine na hata uanpokwenda kununua nguo kwenye mnada utakuta kuna nguo za
mitumba na nguo ambazo si mitumba (special) japo zote ni nguo lakini utakuta bei
zinatofautiana, na hata kwenye mitumba utakuta na yenyewe inazidiana bei
kutegemeana na daraja(grade) la nguo hiyo na ndio maana kuna mitumba daraja la
kwanza, daraja la pili n.k kinachosababisha hayo yote ni kitu kinaitwa
‘THAMANI” kwa hiyo huwezi ukatenganisha THAMANI, HESHIMA NA UPENDO kwa kuwa
kitu chochote chenye thamani kinapendwa na kinaheshimiwa(Isaya 43:4)
Nimeona matangazo na
machapisho mbalimbali yanayofundisha namna ya kuongeza thamani yako katika kazi
au biashara, watu wengi wanaofundisha mambo hayo hufundisha kulingana na uzoefu
au elimu zao, sio vibaya kujifunza ila ukumbuke hiyo ni hekima ya dunia hii na
sio ishukayo kutoka juu kwa hiyo kuna uwezekano wa kuyafanyia kazi hayo
wanayoyafundisha na usione matokeo kwa kuwa ni hekima ya dunia hii.
Suala la kuongeza thamani
yako kwa Mungu ni suala nyeti sana na limo ndani ya biblia na kutokana na hilo
nami napenda kuzungumzia mambo kadhaa yatakayokufanya uongeze thamani yako kwa
Mungu, kumbuka “ukiongeza thamani yako kwa Mungu, Mungu anakuletea watu
unaowahitaji katika eneo Fulani.
Yafuatayo ni mambo
yatakayofanya thamani yako iongezeke kwa Mungu
1.Yesu
kuwa ndani yako(kuokoka)
(Ufunuo 3:20)
Je! wewe unayesoma kitabu
hiki umeokoka au bado? Kama haujampokea Yesu ni vema ujue kuwa thamani yako ni
ndogo sana mbele za Mungu na ndio maana Mungu anakuchukulia kuwa mtu wa kawaida
na tena ameandaa mahali ambapo atawaweka watu wote wanaomkataa Yesu, Thamani
yako itaongezeka pale ambapo utampokea Yesu moyoni mwako na kumkubali atawale
maisha yako.
2.Tembea
katika kusudi la Mungu
Nianze kwa kukuuliza swali
je! unajua kwa nini Mungu alikuumba?
Watu wengi wanamtumikia
Mungu lakini ni wachache wanaomtumikia Mungu sawasawa na kusudi lake kwa hiyo
hata Baraka ambazo watu wengi wanazipata ni Baraka za jumla kumtumikia Mungu
ambazo mtu yeyote anaweza kuzipata, mtu yeyote anayemtumikia Mungu haijalishi
anamtumikia Mungu ndani ya kanisa, serikalini n.k.
Kuna Baraka ambazo mtu
huzipata anapokuwa akimtumikia Mungu katika kusudi lake, hizi ndizo Baraka
maalumu zinazomtofautisha mtu mmoja na mwingine lakini watu wengi hawazipati
hizi kwa kuwa wanamtumikia Mungu nje ya kusudi lake..
Watu wengi na hata
waliookoka wamejikuta wakiishi maisha yasiyo na raha kwa kuwa hawalijui kusudi
la kuumbwa kwao, wamebaki na Yesu lakini hawamtumikii Yesu kulingana na matakwa
ya Yesu, kumbuka kupitia Yesu kila kitu kiliumbwa(Wakolosai 2:16) kwa hiyo
unapookoka lazima ujue ni kwa nini uliumbwa na usipojua kwa nini uliumbwa
utabaki na wokovu lakini hautaona raha ya wokovu kwa kuwa utakuwa unatembea nje
ya mpango wa Mungu na ukitembea nje ya mpngo wa Mungu maana yake ni kwamba
unakuwa hauna nafasi kwenye bajeti ya Mungu na si ajabu hata ukiomba badala ya
Mungu kukupa unachotaka, Mungu anakutumia
neno lake ili likurejeshe kwenye nafasi ili upate msaada na ukitaka kuamini
hili kasome biblia utaona Daudi anasema katika shida yangu nalimwita Bwana na
Bwana alichofanya ni “kumuweka panapo nafasi”(Zaburi 118:5) maana yake
ni kwamba Mfalme daudi alipitia shida kwa kuwa alikuwa nje ya nafasi(kusudi la
Mungu) alipoamua kuomba msaada wa Mungu ilibidi kwanza Mungu amrudishe kwenye
nafasi(kusudi) na ndipo amsaidie.
(2 Wakorintho 7:5-6)
Ukisoma andiko hilo utaona
Paulo alipofika makedonia alijikuta yuko katika dhiki kubwa sana kwa kuwa
alikuwa kwenye mazingira ya hatari na kwa kuwa alikuwa anatumikia kusudi la
Mungu, Mungu alimleta Tito ili kuwafariji katika dhiki hizo, kilichomfanya
Mungu amlete Tito Makedonia ni thamani ya watumishi wake waliokuwa makedonia.
3.Weka
maarifa ndani yako
(Malaki 2:7)
Kila mtu ambaye ameokoka
amefanyika kuhani kwa Mungu kupitia damu ya Yesu(Ufunuo 5:9-10) kwa hiyo
kama biblia inamtaka kuhani ahifadhi maarifa ni kwa sababu watu wanayatafuta
maarifa yatakayowasaidia kufanya mambo mbalimbali, kumbuka huwezi kutafutwa au
kufuatwa na watu kama hawajaona kitu ndani yako kwa hiyo thamani yako
inaongezwa na vitu vilivyomo ndani yako, unapoongeza maarifa ya kiMungu ndani
yako na thamani yako kwa Mungu inaongezeka.
4.Uaminifu
Uaminifu ndio unamfanya
mtu kuwa mwaminifu, hata wewe na mimi tunahitaji watu waaminifu na hata Mungu
pia anahitaji watu waaminifu nan i vema ujue kadri uaminifu wako kwa Mungu
unavyoongezeka ndivyo na thamani yako kwa Mungu inaongezeka.
(Hesabu 12:6-9)
Ukisoma andiko hilo utaona
Mungu akiwashughulikia akina Haruni na Miriamu kwa kuwa walianza vchokochoko
dhidi ya Musa, Mungu aliwashughulikia kwa sababu ya thamani ya Musa mbele zake
na tena akawaambia kuwa Musa ni mwaminifu kwa hiyo tunapata kujua kuwa Mungu
anatahmini sana watu waaminifu kwa gharama zote na hayuko tayari kuwapoteza
watu waaminifu kwake.
5.Tembea
kwenye agano
(Isaya 43:1-4)
Thamani ya taifa la
Israeli ni kubwa sana hata leo na hata mpaka ukamilifu wa dahari kwa kuwa ni
taifa la agano kwa hiyo thamani ya taifa la Israeli haitaweza kupungua mbele za
Mungu kwa kuwa ni taifa la agano ndio maana Mungu anawaambia kuwa wao ni wa
thamani na wa kuheshimiwa na kwa sababu ya thamani yao amewapenda. Ni vema
ufahamu kuwa ukitembea ndani ya agano tahamani yako inakuwa kubwa sana mbele za
Mungu na ndio maana kati ya mambo ambayo Mungu amayazuia ni pamoja na kuvunja
maagano na yeye kwa kuwa unapovunja agano na Mungu unapoteza thamani yako kwa
Mungu kwa kuwa yeye ni Mungu ashikaye magano.
Labda unaweza ukauliza
nini maana ya agano? Jibu rahisi ni kwamba agano ni mapatano kati ya mtu na mtu
au kati ya mtu na Mungu, kwa mfano watu wanapofunga ndoa wanakuwa wameingia
kwenye agano na ikitokea ndoa imekufa maana yake ni kwamba agano limevunjika na
ukifuatilia utakuta hao watu wanachukiana kupita kawaida kwa kuwa agano
linapovunjika na thamani ya uliweka naye agano inapotea.
6.Utii
(Isaya 1:18-19)(Kutoka
19:1-9)
Ni vema ujue kuwa watu
wote ambao huwa wanatii kile ambacho Mungu anakisema thamani yao huongezeka,
yaani kadri unavyoongeza utii wako kwenye neno la Mungu ndivyo na thamani yako
inavyoongezeka mbele za Mungu na kadri unavyoacha kutii neno la Mungu na ndivyo
thamani yako inapungua kwa Mungu, kumbuka kutii ni bora kuliko dhabihu na kuasi
ni kama dhambi ya uchawi(1 Samweli 15:22-23)
Kumbuka unapotii neno la
Mungu maana yake ni kwamba unajifungulia njia ya kula mema ya nje nchi lakini
usipotii unajifungulia mlango wa kuangamia.
7.Uhusiano
wako na Mungu
(Mithali 8:17)
Uhusiano wowote mzuri huwa
unaanza na kutambua thamani, kwa hiyo huwezi kuwa na uhusiano mzuri na mtu au
na Mungu kama haujatambua thamani yake kwako hivyo basi huwezi kumpenda Mungu
kama hautambui thamani ya uwepo wa Mungu kwako, yeye(Mungu) amesema kuwa
anawapenda wale wanaompenda na wale wanaomtafuta kwa bidii watamuona maana yake
ni kwamba anawatahamini wanaomthamini kwa kuwa wale wanaomthamini ndio
wanaomtafuta kwa kuwa wamejua umuhimu wake katika maisha yao kwa hiyo ukiona
mtu anakuwa mgumu kumtafuta Mungu maana yake ni kwamba haoni thamani ya Mungu
katika maisha yake.
Uhusiano wako na Mungu
unakufanya uongeze thamani yako na Mungu, hivyo basi kadri uhusiano wako na
Mungu unavyoongezeka na thamani yako kwa Mungu inaongezeka na thamani yako kwa
Mungu inapoongezeka, Mungu hatashindwa kukuinulia watu wa kusimama pamoja na
wewe kwenye mambo mbalimbali.
8.Kuwa
na siri za Mungu
Jaribu kufikiria watu
ambao wana siri zako, nina uhakika hao watu unawathamini sana ili wasije
kuvujisha hizo siri mahali ambapo hutaki siri zako zivuje. Na Mungu vivyo hivyo
anapoweka siri zake kwa mtu ghafla huyo mtu anaongezeka thamani mbele zake na
Mungu anakuwa tayari kumlinda mtu huyo kwa gharama zozote, na sikuzote siri za
Munguziko kwao wanaomtafuta Mungu ukiona mtu amejikita kumtafuta Mungu ni vema
ujue hata ulinzi wake ni ulinzi wa hali ya juu sana,, na hapa nataka
nikutafakarishe, hapa duniani mifumo ya ulinzi huwa inatofautiana kutegemeana
na kile ambacho kinalindwa, kwa mfano huwezi ukalinganisha ulinzi uliopo benki
na ulinzi walionao wafanyakazi wa benki, wafanyakazi wa benki wanakuwa kwenye
usalama wa kutosha wanapokuwa ndani ya benki lakini wanapotoka eneo la kazi
ulinzi waliokuwa nao kule benki unapungua kwa kuwa kilichowafanya wawe kwenye
usalama wa kutosha ni zile fedha zilizomo na zinazoingia ndani ya benki ambazo
wao huzipokea, hata ulinzi wa Mungu juu ya watu unatofautiana kutegemeana na
mtu husika yukoje mbele za Mungu, kinachomfanya mtu anakuwa na ulinzi mkubwa wa
Mungu ni thamani yake mbele za Mungu.
(2 Wafalme 6:8-17)
Ukisoma andiko hilo utaona
Mfalme wa shamu alikuwa akifanya vita na taifa la Israeli lakini mikakati yake
yote ilifunuliwa na Mungu kupitia mtumishi wa Mungu Nabii Elisha, Mfalme wa
shamu alipojua kuwa kuna mtu anavujisha mambo yake ya siri aliandaa jeshi kubwa
kwenda kumshughulikia Elisha lakini hawakujua kuwa Mungu alikuwa amemuwekea
Elisha ulinzi mkubwa sana na lile jeshi lilipofika kwa Elisha mwishowe
walijikuta wamepigwa upofu na wakajikuta wako kwenye kambi ya wana wa Israeli.
Elisha aliwekewa ulinzi mkubwa kiasi hicho Kwa sababu ya THAMANI yake mbele za
Mungu kwa kuwa ni mtu ambaye alikuwa amebeba siri nyingi za Mungu kwa hiyo
Mungu hakuruhusu mtu yeyote amguse.
5 Maoni
Ooohoo!!! Halekuya!!!!
JibuFutaNeema ya Mungu ktk KRISTO YESU MWOKOZI iongezwe mara dufu kwako. Amen!!
Ooohoo!!! Halekuya!!!!
JibuFutaNeema ya Mungu ktk KRISTO YESU MWOKOZI iongezwe mara dufu kwako. Amen!!
Amen
FutaThanks God
JibuFutaHalo watu wote, jina langu ni Marvelyn Larry. Kwa muda mrefu, mume wangu alikuwa akiishi katika ghorofa nyingine kutokana na shinikizo la kazi na tulifurahi sana pamoja ingawa alikaa mbali nasi kwa miezi kadhaa. Sikujua mwenzangu wa kazi tayari alikuwa na uhusiano naye jambo ambalo lilimfanya mume wangu anipe talaka bila kutarajia. Nilijua kuna kitu kibaya kwa sababu hatukuwahi kupigana au kubishana kiasi hicho ili kumfanya aondoke. Nilikuwa na kiwewe na natafuta msaada wa kukabiliana na hali hiyo iliyonipeleka kwa DR DAWN kutokana na sifa walizomwagiwa na watu mtandaoni. Tulizungumza kwa kirefu na aliniambia kila kitu nilichohitaji kujua kuhusu kile kilichotokea na utaratibu unaofaa wa kurekebisha matatizo. Alitimiza ahadi zake na kumrudisha mume wangu kwangu na mchakato wa talaka ukafutwa. Sasa mume wangu amerudi nyumbani kwetu na tuna furaha pamoja. Inashangaza sana jinsi watu wanaweza kusaidia watu wengine wakati wanahitaji. Anaweza kukusaidia pia. Mtumie tu ujumbe kupitia WhatsApp: +2349046229159
JibuFutaBarua pepe: dawnacuna314@gmail.com