Kwa mfano; ukiwauliza watu waliofanikiwa kwenye maeneo mbalimbali walifanikiwaje? hawatakuambia ukweli au watakuambia ukweli ambao sio mkamilifu si ajabu watakujibu kwamba NI KUJITUMA, KUTOKATA TAMAA, KUSOMA KWA BIDII, KUKUBALI KULIPA GHARAMA NAKADHALIKA lakini ukweli mkamilifu ni kwamba HAKUNA ANAYEFANIKIWA KWENYE DUNIA HII BILA NGUVU YA ZIADA NYUMA YAKE (NGUVU ZA MUNGU AU ZA GIZA).
Ukisoma Biblia utaona Mungu aliwazuia wana wa Israeli wasiseme ni nguvu zao ndizo zimewafanikisha, alitaka watambue kuwa ni nguvu zake ndizo zimewafanikisha katika mambo yao (KUMBUKUMBU LA TORATI 8:17-18)
Kila mtu aliyefanikiwa kwa njia yoyote haijalishi ni njia ya halali au ya haramu ANAYO SIRI MOYONI MWAKE ANAYOJUA ILIYOPELEKEA YEYE KUFANIKIWA.
Kuna wakati Mtume Petro alimwambia Yesu "tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha lakini hatukupata kitu lakini walipomsikiliza Yesu anasema nini ndipo walifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana (LUKA 5:5-6).
NB:
1. Mafanikio sio matokeo ya kazi pekee, kuna watu wanajituma sana, wanafanya kazi kwa bidii sana lakini hawafanikiwi, KAMA HAKUNA NGUVU YA ZIADA NYUMA YAKO HUWEZI KUFANIKIWA KATIKA JAMBO LOLOTE.
2. Shetani akikupa nguvu zake zikufanikishe mwishowe utapatwa na mauti, aibu na mambo mengine mabaya hivyo basi MTAKE MUNGU NA NGUVU ZAKE.

0 Maoni