Sehemu kuu mbili za somo
v Ukweli kuhusu macho ya kiroho
v Namna macho ya kiroho ynavyoweza kufumbuka
UWELI KUHUSU MAMBO YA KIROHO
· Kila mtu ana macho ya aina mbili, macho ya kimwili na macho ya kiroho.
(2 Wafalme 6:15-17) Nabii Elisha hakumuombea mtumishi wake apewe macho ya kiroho bali aliomba Mungu amfumbue macho ilia one, maana yake ni kwamba alikuwa na macho ya kiroho lakini yalikuwa yamefumbwa.
(Mwanzo 21:14-19) Hajiri alikuwa na macho ya kiroho lakini yalikuwa yamefumbwa ndio maana kuna mambo alikuwa hawezi kuyaona, Mungu hakumpa macho bali alimfumbua macho yake.
(Zaburi 119:18) Mfalme Daudi hakuomba apewe macho bali aliomba afumbuliwe macho yake, alitambua ana macho lakini hayajafumbuliwa.
· Macho ya kiroho yanaweza kufumbwa au kufumbuliwa.
Macho ya kiroho yanaweza kufumbwa na Mungu, mtu mwenyewe na shetani, Mungu anaweza kuyafumbua macho ya mtu pia mtu anaweza kuyafumbua macho yake ya kiroho.
(2 Wafalme 6:15-17) Mungu aliyafumbua macho ya mtumishi wa Nabii Elisha.
(Luka 24:13-16) Mungu aliyafumba macho ya wale watu ili wasimtambue Yesu kwa haraka.
(Mwanzo 21:14-19) Hajiri alikuwa na macho lakini yalikuwa yamefumbwa, yalipofumbuliwa akaona maji.
(Mathayo 13:15) Yesu alisema hao watu wameyafumba macho yao maana yake ni kwamba wao wenyewe waliyafumba macho yao, unaweza ukajiuliza waliyafumba kwa namna gani, hao watu waliyafumba macho yao kwa KUTOKUAMINI, jambo mojawapo linalosababisha macho ya mtu ya kiroho yasione ni kutokuamini, imani hutuwezesha kuona “ni bayana ya mambo yasiyoonekana” Waebrania 11:1)
NAMNA MACHO YA KIROHO YANAVYOWEZA KUFUMBUKA
· Kumuomba Mungu akufumbue macho au kuwaombea wengine Mungu awafumbue macho.
(2 Wafalme 6:15-17) Nabii Elisha alimuombea mtumishi wake, Mungu aliyafumbua macho ya mtumishi wa Nabii Elisha.
(Zaburi 119:18) Mfalme Daudi alijiombea Mungu amfumbue macho yake.
· Macho ya kiroho hufumbuka tunapolala usingizi (Mwanzo 28:10-16)
· Kwa kutafakari (Hagai 1:1-7) kutafakari hufumbua macho ya kiroho, baadhi ya watu waliogundua siri kuhusu kutafakari ni Isaka (Mwanzo 24:13) Mfalme Daudi (Zaburi 63:6) (Zaburi27:4) (Zaburi119:97) (Zaburi5:1)
· Weka neno la Mungu kwa wingi ndani yako (Waebrania 4:12-13)
· Jizoeze kuomba katika Roho – kunena kwa lugha kwa Roho Mtakatifu (Waefeso 6:18)
· Amini kile ambacho Mungu amesema (Waebrania 11:1) kuamini ni kuona mambo ambayo hayajatokea katika ulimwengu wa mwili, imani humwezesha mtu kuona, imani hufumbua macho ya kiroho ya mtu.
HITIMISHO
Yapo mambo mengi yanayoharibu macho ya rohoni, jambo mojawapo ni rushwa (Kutoka 23:8)(Kumbukumbu la torati 16:19)(1 Samweli 12:3)
0 Maoni