UKWELI KUHUSU SADAKA YA UKOMBOZI

 

Sadaka za ukombozi katika agano la kale

(Kutoka 30:11-16)

Sadaka za ukombozi katika agano la kale zilitolewa kwa upatanisho yaani kuwapatanisha watu na Mungu, sadaka ziliztolewa na watu wenye umri kuanzia miaka ishirini na kuendelea.

Sadaka za ukombozi zilitumika kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania (Kutoka 30:16).

Sadaka ya ukombozi katika agano jipya

Ukombozi maana yake ni msamaha wa dhambi (Wakolosai 1:14)(Waefeso 1:7)

Sadaka ya ukombozi ni damu ya Yesu Kristo (1 Petro 1:18-19)(Waefeso 1:7)

Je! Ni sahihi kutoa sadaka ya ukombozi

Hatupaswi kutoa sadaka ya ukombozi kwa kuwa sadaka ya ukombozi imeshatolewa na Mungu kwa ajili yetu, sadaka ya ukombozi ni damu ya Yesu (1 Petro 1:18-19)(Waefeso 1:7)

Chapisha Maoni

0 Maoni