NCHI KAMA KIUNGO

 

(Mwanzo 1:1)

UTANGULIZI

Nchi ni kama viungo vya mwili, kila kiungo cha mwili kinahitajika ili mwili ufanye kazi vizuri vivyo hivyo  hili kila nchi ni kiungo cha nchi zingine inapaswa kunufaisha nchi zingine.

Nchi moja ikipata tatizo, tatizo hilo linaweza kuathiri nchi nyingine au nchi zingine kwa mfano kulipozuka virusi vya corona kule China, tatizo lile halikuathiri China peke yake bali liliathiri karibu nchi zote duniani.

Vivyo hvyo nchi moja inaweza kuwa chanzo cha usitawi na maendeleo ya nchi zingine (Mwanzo 41:57) kwa mfano wakati fulani paliwahi kutokea tatizo la njaa duniani, nchi ya Misri ndio nchi pekee ilikuwa na chakula cha kutosha, nchi ya Misri ilikuwa msaada kwa nchi zingine duniani.

ILI NCHI IWE KIUNGO CHENYE MANUFAA KWA VIUNGO (NCHI) VINGINE

a). Lazima nchi itambue yupo Mungu na ikubali neno la Mungu katika nchi hiyo

(Mwanzo 41:31-37) paliwahi kutokea tatizo la njaa duniani, nchi ya Misri ndio nchi pekee ilikuwa na chakula cha kutosha kwa sababu nchi ilikubali kuongozwa na Mungu, mipango ya uhifadhi wa nafaka ulitolewa na Mungu kupitia Yusufu, ilipofika miaka ya njaa watu walitoka nchi mbalimbali kuja kununua chakula pale Misri.

b). Lazima nchi itambue yupo Mungu aliyeiumba

(Matendo ya mitume 17:26) nchi lazima itambue yupo Mungu muumbaji wa mbingu nan chi (Mwanzo 1:1)

c). Lazima nchi ijione kama kiungo cha nchi zingine.

 

 

Chapisha Maoni

0 Maoni