NAFASI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUPATIA MAHITAJI YA KIMWILI


 

UTANGULIZI

Kila mtu ana mahitaji ya kimwili nay a kiroho, Mungu hutupatia mahitaji ya kiroho na ya kimwili tena Biblia imeweka wazi kuwa Mungu anajua tunayoyahitaji (Mathayo 6:25-34)

Watu wengi hudhani Roho Mtakatifu hujishughulisha na mambo ya kiroho tu kama vile kutupatia karama, nguvu nakadhalika, Biblia imeweka wazi kuwa Roho Mtakatifu hujihusisha na mahitaji yetu ya kimwili kabisa sio ya kiroho tu.

ROHO MTAKATIFU NA MAHITAJI YA KIMWILI

1.    Mahitaji ya wana wa Israeli (Hesabu 11:31-32)

Wana wa Israeli walitaka kula nyama, upepo ulitoka mbinguni ukaleta kware. Upepo ulimwakilisha Roho Mtakatifu, unaweza kuona kilichotokea siku ya Pentekoste (Matendo ya mitume 2:1) kwa hiyo Roho Mtakatifu ndiye aliyewaletea kware (nyama) wana wa Israeli.

2.    Mahitaji ya wakristo maskini wa Yerusalemu (Matendo ya mitume 4:34-37)

Roho Mtakatifu ndiye alikuwa anawagusa watu wanauza walivyonavyo na wanaleta fedha ili kuwagawia wakristo maskini. Usidhani ni jambo la kawaida mtu kuuza kiwanja chake halafu pesa yote akagawia watu wengine ambao sio ndugu zake wa damu na hata kama ni ndugu zake wa damu si kila mtu anaweza kufanya hivyo, ni Roho Mtakatifu alikuwa akisababisha hayo kutokea.

HITIMISHO

Roho Mtakatifu tumeona jinsi anavyosababisha watu wapate mahitaji yao ya kimwili kabisa, hivyo basi tusimzimishe Roho Mtakatifu tutapata manufaa makubwa sana katika jamii, nchi nakadhalika.

Chapisha Maoni

0 Maoni