Faraja Gasto
(Luka
18:10-14)
Yapo
mambo mengi ambayo shetani huyafanya wakati mtu au watu wakiwa katika maombi,
jambo mojawapo ni KUTEKA MOYO WA MTU.
Ukisoma
hilo andiko utaona watu wawili walikwenda kusali lakini mmoja alijikuta
ametekwa bila yeye kufahamu kuwa moyo wake umeshatekwa, shetani alipouteka huo
moyo akaujaza kiburi, ona maneno yaliyoanza kutoka kinywani mwake, "Mungu
nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, majambazi, wadhalimu, wazinzi
au kama huyu mtoza ushuru, mimi nafunga mara mbili kwa wiki pia natoa fungu la
kumi" huyo jamaa akaanza kujihesabia haki huku akidhani anaomba.
Watu
wengi wamejikuta wanatekwa na shetani bila wao kufahamu, wengine kwenye maombi
huwa wanajikuta wanajilaani "ooh Bwana mimi ni mdudu tu, mimi sistahili,
mimi ni kama mbwa", wengine hujihukumu, hulalamika, humkemea Yesu n.k
Shetani
ni mwingi wa hila, unahitaji kuwa makini sana ili usitekwe wakati wa maombi.
Ukiwa
kwenye maombi halafu unajikuta unaingiwa na uchovu, mawazo hasi, kumbukumbu
fulani, kupoteza ujasiri n.k fahamu kuwa shetani anataka auteke moyo wako ili
uache kuomba na hata kama utaendelea kuomba, ukosee katika kuomba.
Ili
usitekwe fanya yafuatayo;
1.
Mruhusu Roho Mtakatifu akuongeze kuomba kama atakavyo.
2.
Usiruhusu shetani autumie ufahamu wako kukupitishia mawazo, kumbukumbu, picha
n.k ambavyo vitakufanya upoteze ujasiri wa kuomba au uombe huku moyo wako
unatangatanga huku na kule.
3.
Jifunze kuomba kwa kutoa sauti, usipende kuomba kwa kunong'ona, omba kwa
kunong'ona endapo upo kwenye mazingira yasiyokuruhusu kuomba kwa sauti.
Barikiwa.
0 Maoni