(YAKOBO3:3-11)
UTANGULIZI
Kuutawala ulimi ni kuhakikisha unadhibiti ulimi wako ili usiwe chanzo cha kukuingiza kwenye matatizo.
Watu wengi wamejikuta wamepatwa na matatizo mbalimbali kutokana na kushindwa kutawala ndimi zao, baadhi ya matatizo hayo ni kupigwa, kuuawa, kufukuzwa, kupoteza wateja kwenye biashara, ndoa kuvunjika nakadhalika.
DALILI ZA MTU ALISHINDWA KUTAWALA ULIMI WAKE
1. Matukano na matusi (Wakolosai 3:8)
2. Maneno machafu (Waefeso 4:29)
3. Kutojua namna ya kujibu (Wakolosai 4:6) Kaini aliulizwa yuko wapi ndugu yako Habili? Lakini Kaini alijibu kuwa “mimi sio mlinzi wa ndugu yangu” Mwanzo 4:6
MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU ULIMI
1. Ulimi unaweza kusababisha ukapatwa na mema au mabaya (Hesabu 14:26)
2. Mungu hutekeleza unachokiri (Isaya 57:19-21)
3. Ulimi unaweza kukuingiza kwenye taabu (Mithali 21:23)
4. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi (Mithali 18:20-21)
5. Ulimi unaweza kupanda mema au mabaya (Mithali 6:16-19)
MAMBO YA KUKUSAIDIA ILI KUUTAWALA ULIMI
1. Weka neno la Mungu kwa wingi moyoni mwako (Wakolosai 3:16)
2. Omba Mungu akupe hekima na maarifa ya kutumia ulimi wako (Mithali 2:6)
0 Maoni