ADHABU KUTOKA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO

 

Mambo ya kujifunza katika somo hili

v Hukumu

v Aina za adhabu

v Utekelezaji wa adhabu

v Mambo ya kufanya ili kuondokana na adhabu

UTANGULIZI

Sikumoja kijana mmoja alinifuata akitaka nimuombee, kijana yule alikuwa amepooza miguu anatembea akiwa na fimbo ya kumsaidia asianguke, alipokuja nikaanza kumfundisha neno la Mungu kabla ya kumuombea, nilimuombea kwa muda mfupi kisha akaondoka.

Baada ya hapo nilitenga muda wa kumuomba Mungu aniongoze namna gani nitamuombea yule kijana ili apate uponyaji, wakati namuuliza Mungu nimuombee vipi yule kijana ndipo Mungu aliponifunulia kuhusu suala la “adhabu kutoka kwenye ulimwengu wa roho”

Ifahamike kuwa katika ulimwengu wa mwili watu hupewa adhabu na mahakama, wazazi, waalimu nakadhalika kutokana na makosa ambayo mtu ameyatenda.

Vivyo hivyo katika ulimwengu wa roho huwa zinatoka adhabu mbalimbali ambazo Mungu au shetani huwaadhibu watu kutegemeana na sababu mbalimbali.

KIPENGELE CHA KWANZA: HUKUMU

Mungu hutoa hukumu (Yohana 5:27)(Ufunuo wa Yohana 19:11) pia shetani naye hutoa hukumu (1 Timotheo 3:6)

Hukumu huwa ina matokeo ya aina mbili tu

v Haki (kuhesabiwa haki)

v Adhabu (endapo utakutwa na hatia)

Kwa hiyo hukumu ndio inazaa adhabu, ikiwa kuna mtu ameadhibiwa ni kwa sababu tayari amekutwa na hatia.

KIPENGELE CHA PILI: AINA ZA ADHABU KUTOKA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO

Kuna aina kuu mbili za adhabu ambazo ni;-

v Adhabu kutoka kwa Mungu

v Adhabu kutoka kwa shetani

Adhabu kutoka kwa Mungu

Mungu huwaadhibu watu kwa namna mbalimbali (2 Samweli 7:14), Mungu huadhibu mtu, watu, taifa, eneo nakadhalika. Baadhi ya aina za Mungu kutoka kwa Mungu;-

v Adhabu ya tauni (2 Samweli 24:10-15)(Hesabu 14:36)

v Adhabu ya kifo (Mwanzo 6:5-7)

v Adhabu juu eneo fulani (Mwanzo 19:24-25)

v Adhabu ya ukoma (Hesabu 12:9-10)

v Adhabu ya kutangatanga (Mwanzo 4:13-14)(Zaburi 107:4) kuna watu wamekuwa wanatangatanga hawawezi kutulia sehemu moja, hawawezi kutulia kwenye ndoa, hawawezi kutulia kwenye kanisa kwa mwaka mmoja mtu anaweza kuhama kwenye madhehebu tofauti tofauti n.k

Adhabu kutoka kwa shetani

Shetani naye huwaadhibu watu ambao wako kinyume naye, waliokaidi utaratibu wake nakadhalika. Baadhi ya adhabu kutoka kwa shetani;-

v Adhabu ya vifungo (Waamuzi 16:21), kuna aina nyingi za vifungo kama vile vifungo vya taabu (Zaburi 107:10) yaani mtu anakuwa na taabu sikuzote, vifungo vya mwili (Marko 7:31-35)(Luka 13:16) miguu inaweza kufungwa, tumbo la uzazi linaweza kufungwa nakadhalika, kuna vifungo vya nafsi mtu anakuwa haelewi hata akifundishwa, mtu anakuwa anasahau kwa haraka sana nakdhalika.

v Adhabu ya kifo (Danieli 3:1-16)(1 Wafalme 19:1-3)

v Adhabu ya utumwa (Waamuzi 16:21)

KIPENGELE CHA TATU: UTEKELEZAJI WA ADHABU KUTOKA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO

Utekelezaji wa adhabu za Mungu

Mungu hutumia njia nyingi kutekeleza adhabu zake, baadhi ni hizi zifuatazo

v Mungu hutumia malaika kutekeleza adhabu ambazo amezitoa (2 Samweli 24:15-17)(Mwanzo 19:1)

v Mungu hutumia watu kuwaadhibu watu (Esta 7:7-10)(Yeremia 50:8-10)

v Mungu hutumia viumbe vingine kama moto, maji, upepo, wanyama nakadhalika (Mwanzo 19:24-25)(Mwanzo 7:17-24)(1 wafalme 13:23-25).

Utekelezajiwa adhabu za shetani

Shetani hutumia njia nyingi kutekeleza adhabu zake, baadhi ni hizi zifuatazo

v Shetani hutumia pepo

v Shetani hutumia watu

v Shetani hutumia viumbe wengine kama vile upepo, moto , wanyama n.k (Ayubu 1:13-19)

KIPENGELE CHA NNE: MAMBO YA KUFANYA ILI KUONDOKANA NA ADHABU

Kuondokana na adhabu za Mungu

v Omba Mungu akusamehe kwa kukaidi maagizo yake na kwa kukaidi maonyo aliyokupa kabla hajatoa adhabu (Danieli 9:4-21)

v Omba Mungu afute hukumu iliyosababisha akaachilia hiyo adhabu juu yako, juu ya eneo nakadhalika (Warumi 8:1).

v Omba Mungu awaachishe kazi aliowapa kutekeleza hukumu hiyo ili waache kuitekeleza (2 Samweli 24:16-17)

 

Kuondokana na adhabu za shetani

v Okoka kama haujaokoka (Warumi 8:1)(Warumi 10:9-10)

v Kama umeokoka omba Mungu akusamehe kwa ajili ya mambo uliyonkosea yaliyopelekea shetani akapata nafasi ya kukuadhibu

v Tumia damu ya Yesu kufuta na kuondoa hati ya mashitaka ambayo shetani anayatumia kukuadhibu au kutoa adhabu (Wakolosai 2:14)

v Kemea waliotumwa kutekeleza adhabu hizo.

 

 

Chapisha Maoni

0 Maoni