JUHUDI BILA MUNGU


 Usitake kuniambia Ibrahimu na mkewe Sara walikuwa hawakutani kimwili, ni hakika walikuwa wanakutana kimwili lakini hawakuwahi kupata mtoto mpaka Mungu aliposema mwakani Sara atazaa "Ndipo Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’  Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Bwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.” MWANZO 18:13-14

Usitake kuniambia Petro alikuwa hana uzoefu wa kuvua samaki, ni hakika uzoefu alikuwa nao lakini kuna wakati alikosa samaki mpaka Yesu aliposema neno "Simoni akamjibu, “Bwana, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu. LUKA 5:5

IKO HIVI: Juhudi zetu hazitoshi kutufanikisha bali MUNGU tu ndiye anayeweza kutufanikisha, tunapompa Mungu nafasi katika maisha yetu na mambo yetu huwa yanafanikiwa kwa wepesi bila kutumia nguvu nyingi kwa kuwa Mungu hutusaidia.

Wakati mwingine watu wanatumia nguvu nyingi na gharama kubwa kufanya mambo mbalimbali kama vile Petro alivyomwambia Yesu "tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha hatujapata kitu" lakini neno la YESU liliwafanikisha kwa muda mfupi bila kutumia nguvu nyingi.

HITIMISHO

Ni vema kila mtu afahamu kuwa juhudi bila Mungu ni sawa na kukimbiza upepo hivyo basi mtake Mungu kwenye maisha yako na mambo yako.

Chapisha Maoni

2 Maoni