UTANGULIZI
Hapa duniani kuna vitu ili uvipate lazima uchimbe kwa mfano uchimbaji wa madini, uchimbaji wa mafuta, uchimbaji wa gesi, uchimbaji wa maji (Kutoka 7:24)(Mwanzo 26:19-22) nakadhalika.
Hivyo basi kwa mifano hiyo inatupa kufahamu kuwa kuna vitu ili tuvipate lazima tuchimbe.
KUCHIMBA MAMBO YA KIUNGU
Vivyo hivyo kwenye mambo ya kiungu (mafunuo, nguvu za Mungu nakadhalika), kuna mambo ili tuyapate lazima tuchimbe
1.Tuchimbe kwa maombi.
2.Tuchimbe kwa kusoma neno la Mungu pia kusoma vitabu mbalimbali hususani ambavyo vimebeba maarifa kutoka kwa Mungu au vitabu ambavyo vimeandikwa na watumishi wa Mungu.
HITIMISHO
Usipokuwa tayari kuchimba, kuna mambo ya kiungu hautayapata kabisa utakuwa unayasikia kama hadithi hivyo basi amua kuwa mchimbaji.
0 Maoni