Faraja Gasto ✍️✍️✍️
UTANGULIZI
Tarehe 4 mwezi wa kwanza mwaka 2009 (4/01/2009) mwili wa Kristo ulipoteza kiungo muhimu sana hususani katika huduma ya uimbaji kutokana na kufariki kwa ndugu yetu FANUEL SEDEKIA.
Fanuel Sedekia ni mojawapo ya waimbaji wa nyimbo za injili ambao huduma yake inaendelea kuwa baraka sana hata kwa wakati huu ambao amelala katika Bwana.
UTAFITI WANGU
Binafsi ninafahamu nyimbo 60 za ndugu yetu Fanuel Sedekia, nyimbo hizo zimeimbwa kwa kutumia funguo za muziki 9 ambazo ni F, F#, C, A, G, B, D, D#, E.
Nyimbo 22 zimeimbwa kwa ufunguo F
Nyimbo 2 zimeimbwa kwa ufunguo F#
Nyimbo 9 zimeimbwa kwa ufunguo C
Nyimbo 10 zimeimbwa kwa ufunguo A
Nyimbo 10 zimeimbwa kwa ufunguo G
Nyimbo 2 zimeimbwa kwa ufunguo D
Nyimbo 1 umeimbwa kwa ufunguo D#
Nyimbo 3 zimeimbwa kwa ufunguo E
Nyimbo 1 umeimbwa kwa ufunguo B
NILIYOBAINI KWENYE UTAFITI WANGU
1.Fanuel Sedekia alikuwa anajithamini ndio maana nyimbo nyingi aliziimba kwenye ufunguo "F" ambayo ni herufi ya mwanzo ya jina lake.
2.Nyimbo zake zimeendelea kuwa baraka sana kwa kuwa alikuwa mtu wa tabia ya rohoni.
HITIMISHO
Katika msiba huo, mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege alipata nafasi ya kuzungumza mambo mengi ya muhimu, alimalizia kwa kuwasihi watu wote walioguswa na msiba ule, kila mtu ajiulize maswali haya matatu na apate jibu lake
(Ninamnukuu)
1. Kwanza jiulize, ukifa unataka ukumbukwe kwa lipi?
2. Baada ya kifo, zipo sehemu mbili tuu za kwenda, mbinguni na jehanam, je unataka ukifa uende wapi?
3. Je, Yesu Kristo akirudi leo, utanyakuliwa na Yeye au utabaki?
(Mwisho wa kunukuu)
0 Maoni